Na Mwandishi Wetu
Posted Jumanne,Marchi18 2014 saa 19:4 PM
Posted Jumanne,Marchi18 2014 saa 19:4 PM
Kwa ufupi
Dodoma. Mwenyekiti wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesisitiza kuwa mapendekezo
ya serikali tatu katika Muungano ni ya wananchi na taasisi mbalimbali,
na wala si matakwa ya tume yake.
Akiwasilisha Rasimu ya Pili ya Katiba wakati wa
kikao mahsusi cha Bunge Maalum mjini Dodoma, Jaji Warioba alieleza kuwa
nusu ya wananchi waliotoa maoni yao kuhusu Muungano walitaka uwepo wa
serikali tatu.
Kati ya wananchi 38,000 waliotoa maoni yao kuhusu
Muungano, 19,000 walizungumzia suala la muundo, huku zaidi ya nusu
wakitaka marekebisho ya kikatiba yatakayowezesha uwepo wa serikali tatu.
“Kwa upande wa Bara, asilimia 61 [ya wale waliotoa
maoni juu ya Muungano] walipendekeza muundo wa serikali tatu,” alisema
Jaji Warioba. “Kwa upande wa Zanzibar, [asilimia] 60 walipendekeza
Muungano wa mkataba.”
Tazama VIDEO uone mengine yalojiri Dodoma leo.
0 comments :
Post a Comment