Sumaye akata rufaa kupinga adhabu ya kamati kuu ya CCM .

sumayeclip_5756f.jpg
Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye
Dodoma. Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye amekata rufaa Kamati Kuu ya CCM kupinga adhabu ya onyo kali aliyopewa na chama kutokana na madai ya kuanza kampeni za urais mapema kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu ujao. Akizungumza na gazeti hili mjini Dodoma jana, Sumaye alisema kwa ufupi hakuridhishwa na adhabu hiyo na kuthibitisha hilo, tayari amekata rufaa. Hata hivyo, alisema hadi jana hakuwa amepata mrejesho wowote kwa sababu kanuni hazielezi ni muda gani anatakiwa kuwa amepewa taarifa kuhusu rufaa hiyo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment