Diamond akiwa ndani ya Toyota Land Cruiser V8 linalopigwa bei kwa sasa.
LILE
gari aina ya Toyota Land Cruiser V8 alilokuwa akitanua nalo staa wa
muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ liko sokoni linapigwa bei.
Gari
hilo linalomilikiwa na pedeshee maarufu Bongo, Mohammed Kiumbe ‘Chief
Kiumbe’ limewekwa sokoni baada ya staa huyo kuchemsha kutoa fedha za
kulinunua pamoja na kupewa muda wa kufanya hivyo.
Wengi
waliamini na kumweka Diamond au Sukari ya Warembo katika matawi ya juu
kutokana na kumiliki gari hilo lenye thamani kubwa na lililojaa
vikorombwezo vingi ndani yake.
Staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Picha
za Diamond akiwa ndani ya gari hilo zilionekana kwenye magazeti huku
akikaririwa kwamba analimiliki kihalali gari hilo aina ya Toyota
Landcruiser V8 lenye thamani ya shilingi milioni mia moja na laki moja
(100,100,000).
Siku
chache zilizopita, Chief Kiumbe alimnyang’anya Diamond gari hilo kwa
kile kilichodaiwa kuwa staa huyo alishindwa kutoa ‘mpunga’ wa kulinunua
pamoja na kukaa nalo kwa muda mrefu.
Baada
ya hapo gari hilo likapotea machoni mwa watu kwa kutojulikana
lilipokuwa limefichwa ingawaje ilidaiwa kuwa Chief Kiumbe alikuwa
ameliweka stoo.
...Gari hilo likiwa sokoni.
Mapaparazi
wa Risasi Mchanganyiko walilitafuta gari hilo kwa udi na uvumba, ndipo
walipobaini kwamba lilikuwa limewekwa sokoni katika yadi moja iliyopo
maeneo ya Kijitonyama, Dar likipigwa bei.
Waandishi wetu walifika katika yadi hiyo na kujifanya wanunuzi na kuambiwa kuwa gari hilo lilimshinda Diamond.
“Hili
gari lina vitu vingi vizuri, ukiwa na ‘sensa’ ndipo unapoweza kuondoka
nalo kwa sababu halitumii funguo, bila hivyo huwezi, Diamond ameshindwa
kulinunua,” alisema jamaa aliyekutwa katika yadi hiyo.
Waandishi
hao walitajiwa bei na kupewa nafasi ya kulikagua gari hilo kila kona,
hatimaye waliondoka ndani ya yadi hiyo wakiahidi kurudi na mkwanja ili
kufanya kile kilichomshinda Sukari ya Warembo.
0 comments :
Post a Comment