Bado siku 77 tuweze kushuhudia fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi na kila shabiki wa soka ana hamu ya kufahamu michuano hiyo ambayo inafanyika mara moja kila baada ya miaka minne, hivyo kuelekea fainali za Kombe la Dunia 2018 naomba nikukumbushe rekodi za Kombe la Dunia zilizopita.
1- Goli la mapema zaidi kuwahi kufungwa katika Kombe la dunia lilifungwa ndani ya sekunde 10.8 baada ya game kuanza, lilifungwa na Hakan Sukur wa Uturuki mwaka 2002 katika game dhidi ya Korea Kusini.
2- Miroslav Klose ameweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa michuano ya Kombe la Dunia kwa kufunga goli lake la 16 akiitumikia Ujerumani na kuvunja rekodi ya Ronaldo De Lima aliyekuwa anashikilia rekodi hiyo kwa kufunga jumla ya magoli 15.
3- Game ya Marekani dhidi ya Ureno katika fainali za Kombe la Dunia 2002 ndio game iliyomalizika kwa magoli mengi ya kufungana, game hiyo kila timu ilijifunga goli katika mchezo huo.
4- Mchezaji mwenye umri mdogo kuwahi kufunga goli katika fainali za Kombe la Dunia ni mkongwe wa Brazil Pele, ambaye alifanya hivyo akiitumikia Brazil akiwa na umri wa miaka 17.
5- Mchezaji mwenye umri mkubwa kuwahi kufunga goli katika fainali za Kombe la Dunia ni Roger Milla, alifanya hivyo akiichezea timu ya taifa ya Cameroon huku yeye akiwa na umri wa miaka 42.
6- Game ya fainali za Kombe la Dunia iliyowahi kuhudhuriwa na watu wengi zaidi ilikuwa mwaka 1950 nchini Brazil katika uwanja wa Maracana, uwanja huo ulihudhuriwa na mashabiki 173,850.
7- Fainali za Kombe la Dunia 2010 zilizofanyika nchini Afrika Kusini ikiwa ndio kwa mara ya kwanza fainali hizo kufanyika Afrika, ziliweka rekodi ya kuwa tukio kubwa la kimichezo kuwahi kufuatiliwa na watu wengi duniani.
0 comments :
Post a Comment