Kwa ufupi
Dar es Salaam. Rais Jakaya
Kikwete amesema kuwa hakuwa na nia ya kuidhalilisha Tume ya Mabadiliko
ya Katiba wakati alipohutubia kulifungua Bunge Maalumu la Katiba, wiki
mbili zilizopita.
Rais Kikwete alisema hayo jana kwenye ziara yake
ya siku tatu ya kidola nchini Uingereza, moja ya ziara nadra kufanywa na
viongozi wa nchi za nje nchini humo.
Alisema kuwa anawaheshimu sana wazee waliokuwa
wanashughulikia mchakato mzima wa kuandaa Rasimu ya Katiba Mpya, hivyo
hakukuwa na sababu ya yeye kuwafanyia jambo hilo.
“Watu wamesema eeeh! umeidhalilisha tume!… Siwezi
kufanya kazi hiyo! Nawaheshimu sana hao wazee ndio walionilea mpaka hapa
nilipofika,” alisema Kikwete.
Alifafanua kuwa hotuba yake ililenga kuwashauri
wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kuangalia kwa kina masuala yaliyomo
ndani ya Katiba ili kufanya uamuzi sahihi.
Wakati akiwasilisha hotuba yake bungeni hivi karibuni, Rais alionekana kutilia shaka takwimu zilizotolewa na tume hiyo.
“Nilitoa maoni yangu ya rasimu kwa sababu ninayo
dhamana hiyo… Wao walitaka niseme; wajumbe nimelizindua Bunge. Hiyo
haiwezekani,” aliongeza Rais Kikwete akiashiria kuwa
0 comments :
Post a Comment