Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora, Sipora Liana.
 |
| Mkurugenzi
wa Manispaa ya Tabora, Sipora Liana, akijieleza mbele ya Baraza la
Maadili kwa Viongozi wa Umma Dar es Salaam leo, alipofikishwa kwa tuhuma
za kukiuka maadili ya viongozi wa umma alipokuwa Halmshauri ya Manispaa
ya Mkuranga mkoani Pwani kabla ya kuhamishiwa Tabora. |
 |
|
Jaji Msumi (katikati), akiwa na wenzake akisikiliza shauri hilo.
Na Dotto Mwaibale
KAMANDA wa Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (Takukuru), Wilaya ya Mkuranga, Damas Pasalau,
amemkingia kifua aliyekuwa Mkurugenzi wa Halamashauri ya Manispaa ya
Mkuranga Sipora Liana kwa tuhuma zinazomkabili katika Baraza la Maadili
ya Utumishi wa Umma.
Kwa mujibu wa hati ya mashitaka
iliyosomwa katika vikao vya baraza a maadili vilivyoanza jana jijini
Dar es Salaam, Sipora ambaye kwa sasa Mkurugenzi wa Manispaa ya Arusha
anakabiliwa na tuhuma za kukiuka maadili.
Inadaiwa kuwa mnamo mwaka
2009/2010 Sipora alimchukulia hatua za kinidhamu bila sababu za msingi
kwa kumsimamisha kazi aliyekuwa Ofisa Kilimo, Mifugo na Ushirika Wilaya
ya Mkuranga Dk. Fransis Mallya kinyume na sheria ya maadili ya utumishi
wa umma.
Pasalaus alitoa utetezi kwa
muda wa dakika 30 ambapo kati ya hizo 10 alizitumia kutoa utetezi wakati
akiulizwa maswali na Mwanasheria wa Serikali Getrude Cyriacus.
Pasalau ambaye mara kwa mara
alibanwa na mwanasheria huyo kwaajiri ya kutoa ushahidi sahihi
aliendelea kumtetea huku akitoa mifano mbalimbali na utendaji kazi wake
uliofanyika katika Wilaya aliyotoka Sipora huku akidai kuwa ni kitendo
hichop ni chuki binafsi hivyo zisiruhusiwe kushika nafasi kwenye mali za
umma.
Wakati akitoa ushahidi huo
alimtaka Jaji Hamis Msumi kutenda haki na kudai kuwa Mkurugenzi huyo
hana kosa bali ni hujuma za baadhi ya watu ambao walikuwa kwa maslahi
yao binafsi katika ofisi za Manispaa hiyo.
Alisema awali katika Manispaa
hiyo kulikuwa na msuguano kati ya Madiwani, watumishi wa umma na
wakurugenzi jambo ambalo baada ya kufanyika kwa uchunguzi na taasisi
hiyo ilibainika uwepo wa ubadhilifu wa mali za umma.
“Baada ya Sipora kuwasili
katika halmashauri hiyo ambapo katika utendaji kazi wake mzuri watu
wengi hawakumpenda kwani wengi wao walikuwa wakifanya shughuli zao kwa
maslahi binafsi,” alisema.
Alidai baada ya Mkurugenzi huyo
kufika na kuonekana utendaji wake unawabana baadhi ya watu akiwemo
Mallya na wenzie waliunda kundi ambalo lilikuwa ni kwaajili ya kupambana
nae.
“Watu hawa walitumia vyombo vya udhibiti wa maadili kutunga hoja za uwongo ili kuweza kufanikisha malengo yao.
” Ila kiukweli mwenyekiti huyu
mama amethubutu na ameweza kulingana na hali ya mazingira yaliyoko
katika halmashauri ile kwatu watendaji wengi hawakupenda watu wa aina
hii,” alisema.
Akifafanua zaidi kuhusu tatizo
lililotokea hadi hatua za kusimamishwa kazi zilipotokea alidai kuwa
baada ya Mkurugenzi huyo kuwasili katika halmashauri hiyo alianza
kufuatilia idara ya Mallya katika kukamilisha miradi ya Mabwawa ya
Mkwalia pamoja na ununuzi wa vitotozi visivyofanyakazi na kuweka
mashamba hewa ambapo hakuwa amefanya kazi yeyote.
Hata hivyo shauri hilo
liliahirishwa kutokana na anaedaiwa kuwa ni mlalamikiwa Sipora, kutofika
na mashahidi wake kama alivyowasilisha idadi yao katika baraza la hilo.
Akihairisha kikao cha baraza
hilo, Jaji Msumi alisema shauri hilo litasikilizwa hadi pale
itakapotolewa hati maalum ya wito kwa mashahidi wa Mkurugenzi huyo.
|
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments :
Post a Comment