ya Biashara, Sabasaba viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam wakiangalia machapisho anuai ndani ya banda hilo
------------------------------------------
WANACHAMA
wote wa NSSF na wasio Wanachama Mnakaribishwa kujionea na kupata huduma
mbalimbali zikiwemo, taarifa za jumla zinazohusu kujiandikisha
uanachama, uwekezaji unaofanywa na Shirika, Maelezo kuhusu Bima ya afya
itolewayo na NSSF,na kupata Kadi mpya.
Wageni
wote wanaweza kujua kuhusu namna ya kuwasilisha maoni yao kupitia mfumo
wetu mypa wa HaapyOrNot uliopo katika ofisi za Kinondoni, Ilala, Temeke
na GDE- Waterfront Kwa kutumia mfumo huo mwanachama na asiye mwanachama
anaweza kutuambia amefurahia huduma au Hapana pindi anapotembelea Ofisi
za NSSF.
Pia
wastaafu wote wanaofaidika na Pensheni za NSSF wataweza kupata pensheni
kupitia mfumo mpya wa HIFADHI SMART ambapo mstaafu ataweza kupata fedha
zake sehemu yoyote.
Vilevile
wanachama na wasio wanachama mnakaribishwa ili muweze kujua kuhusu
Huduma yetu mpya ya HIFADHI FASTA ambayo mwanachama sasa anaweza kulipa
michango yake kupitia mtandao wa SELCOM wireless hivyo kumrahisishia
yeye kuepuka usumbufu wa kutembea umbali mrefu ili aweze kuwasilisha
michango yake.
Nkupamah blog
0 comments :
Post a Comment