Kada wa
CCM, Antony Chalamila (mbele kulia) akitembea kwa miguu wakati ekienda
kutafuta basi la kumrejesha mkoani Morogoro, baada ya kuchukuwa fomu za
kuomba kugombea kiti cha Urais kupitia chama hicho, mjini Dodoma jana.
Picha na Edwin Mjwahuzi.
Antony
Chalamila (66) amekuwa mgombe wa 41 kuchukua fomu ya kuomba kupitishwa
na CCM kuwania urais, lakini kivutio kilikuwa ni jinsi alivyochapa mguu
kutoka ofisi za chama hicho hadi stendi ya mabasi kurudi mkoani
Morogoro.
Wakati
kada huyo akijitokeza tano kabla ya muda wa kuchukua na kurejesha fomu
kuisha, makada wengine wawili walirejesha fomu, huku Balozi Amina Salum
Ali akilalamikia kukithiri kwa rushwa katika mchakato.
Chalamila,
ambaye aliongozana na msaidizi wake Benjamin Ruvunduka kwenda kuchukua
fomu ofisi za makao makuu ya CCM, hakuwa na usafiri wowote wakati wa
kuondoka na hivyo kutembea umbali wa takriban kilomita 1.2 kwenda kituo
cha mabasi kurejea mkoani kwake Morogoro.(P.T)
“Naelekea
Morogoro hivi sasa wananisubiri huko,” alisema Chalamila alipokuwa
akiondoka maeneo ya ofisi hizo huku akisema anashangazwa na kitendo cha
waandishi wa habari kumuuliza sababu za kutotoa taarifa za tukio lake.
Chalamila
alifika ofisi hizo saa 4:15 asubuhi, akiwa amevalia shati la kijani na
suruali nyeusi huku akiwa ameshikilia kifimbo cheusi mithili ya kile cha
Hayati Mwalimu Nyerere.
Tofauti
na wengine, Chalamila alikuwa akizungumza mithili ya Mwalimu Nyerere kwa
kuzungusha midomo na kuitembeza mikono usoni akiwa na kifimbo hicho
ambacho alisema alikinunua Rufiji.
Chalamila
aliwaambia waandishi wa habari kuwa anaomba nafasi hiyo kwa sababu yeye
ni mwanachama wa CCM na miongoni mwa haki zake kikatiba ni kuchagua na
kuchaguliwa.
Alisema bila ubinadamu huwezi kuongoza.
Alipoulizwa
iwapo muda wa siku tano kuanzia jana utatosha wa kutafuta wadhamini,
Chalamila alisema unamtosha na kwamba atatumia teknolojia ya mawasiliano
ya kompyuta kupata wadhamini na maeneo mengine atatembea.
“Siku
zilizobaki siyo chache wala nyingi sana. Sasa hivi vijana tunajifunza IT
(teknolojia ya mawasiliano ya kompyuta). Nitatumia IT na vilevile
nitatembea,”alisema.
“Suala la
kwanini nimekuwa wa mwisho, si tatizo kwa sababu aliyetangulia anaweza
kuwa wa mwisho na wa mwisho akawa wa kwanza,”alisema kada huyo huku
akikicheza kifimbo chake.
Chalamila ni nani?
Chalamila
alizaliwa Oktoba 15 mwaka 1949 na kusoma Shule ya Msingi Kigurunyembe
na baadaye kujiendeleza kama mtahiniwa binafsi hadi kidato cha sita.
Baadaye
alijiunga na Chuo cha Ualimu Chang’ombe jijini Dar es Salaam ambapo
alitunukiwa stashada ya masomo ya uhasibu na biashara. Aliwahi
kufundisha Shule ya Sekondari ya Iliboro mkoani Arusha na Sekondari ya
Morogoro .
Kwa sasa
Chalamila ni meneja mkuu wa Chama cha Ushirika cha Kilimo na Masoko cha
Morogoro na Mvomero na ana shahada ya Elimu aliyoipata Chuo Kikuu Huria
(OUT).
Wanachama wanaomba rushwa
Awali,
Balozi Amina Salum Ali alirejesha fomu zake jana lakini akaungana na
makada wengine kulalamikia rushwa ndani ya CCM akisema kuwa alikumbana
na matatizo kutokana na wanachama kumuomba fedha ili wamdhamini.
Aliwatuhumu makada wengine wanaowania urais kuwa wamekuwa wakitumia
fedha nyingi katika mpango huo wakati kuna wananchi wanashindwa kupata
hata mlo mmoja wa chakula kutokana na hali ngumu ya kiuchumi.
“Kuna
mkoa mmoja baadhi ya wadhamini walitaka kupigana kwa sababu hawakupewa
fedha zao za kusaini fomu...Wakati haya yanatokea ya matumizi makubwa ya
fedha, kuna watu hata milo miwili ni tabu kwao,” alisema.
Balozi
Amina alisema wana-CCM wengine wamediriki hata kutamka kuwa hawatapiga
kura bila kupewa fedha, jambo ambalo linaharibu utu na heshima ya
mwanadamu.
“Chama ni
mapenzi, chama maana yake ni kujenga misingi, chama ni kujitolea,
unataka uongozi ndani ya chama ujitolee. Sisi tumejitolea miaka chungu
mzima sio sasa hivi. Kwa hiyo kweli ni (rushwa) tishio,”alisema.
Katika
hatua nyingine, Jaji Augustino Ramadhani, amesema hatakubali kuungwa
mkono na mgombea wa chama chake mwenye tabia za wizi.
Akizungumza
baada ya kurudisha fomu mjini Dodoma jana, Jaji Ramadhani alisema:
“Atakayenifuata kuomba kuungana na mimi nitamwangalia kwanza. Kama ana
tabia za wizi, siwezi kukubali kuungwa mkono naye lakini kama anatabia
njema nitakubali.”
“Sijaungana
na mtu yeyote, hakuna mtu aliyenifuata wala mimi niliyemfuata.
Nilipokuja kuomba kuchukua fomu nilikuja pekee yangu, nikisindikizwa na
hawa wote ambao nimerudi nao leo (jana),” alisema.
Membe
0 comments :
Post a Comment