- Written by Nkupamah blog

Kocha Mkwasa (kushoto) na msaidizi wake Hemed Morocco wakiongea na waandishi wa habari.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - RELEASE NO. 104
TAREHE 24 JUNI 2015
TAREHE 24 JUNI 2015
Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine
leo amemtambuisha kocha mpya wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)
Charles Boniface Mkwasa mbele ya waandishi wa habari.
Akiongea
na waandishi wa habari, Mwesigwa amewaomba wadau wa mpira wa miguu
nchini kuwapa sapoti makocha hao wazawa wanaoanza kazi kesho kujiandaa
na mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda julai 4, 2015 jijini Kampala.
na mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda julai 4, 2015 jijini Kampala.
Mara
baada ya kutambulishwa kwa waandishi wa habari, Mkwasa amesema
anashukuru kwa TFF kumpatia nafasi hiyo ya kuingoza Taifa Stars na
msaidizi wake Hemed Morocco, na kuomba watanzania kuwapa sapoti.
Mkwasa
amesema cha kwanza atakachokifanya na msaidizi wake Morocco ni kurudisha
imani ya watanzania juu ya timu yao ya Taifa, kisha watajitahidi kadri
ya uwezo wao kuhakikisha kuwa timu inafanya vizuri katika michezo
inayowakabili.
Aidha
Mkwasa ametangaza kikosi cha wachezaji 26 watakaoingia kambini kesho
alhamisi katika hoteli ya Tansoma tayari kwa ajili ya maandalizi ya
mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda.
Wachezaji walioitwa ni makipa: Mudathir Khamis (KMKM), Mwadini Ally (Azam), Ally Mustafa “Barthez” (Yanga).
Walinzi:
Shomari Kapombe (Azam), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Mohamed Hussein
“Tshabalala” (Simba), Haji Mwinyi (KMKM), Nadir Haroub “Cannavaro”
(Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Hassan Isihaka (Simba), Aggrey Morris
(Azam).
Viungo: Jonas Mkude (Simba), Abdi Banda (Simba), Salum Telela (Yanga), Frank Domayo (Azam).
Viungo wa pembeni: Saimon Msuva (Yanga), Said Ndemla (Simba), Deus Kaseke (Mbeya City), Ramadhan Singano “Messi” (Simba).
Washambuliaji: John Bocco (Azam), Atupele Green (Kagera Sugar), Rashid Mandawa (Kagera Sugar) na Ame Ally (Mtibwa Sugar).
Wachezaji
Juma Abdul (Yanga), Mudathir Yahya (Azam) na Samwel Kamuntu (JKT Ruvu)
wameitwa kama wachezaji wa akiba katika kikosi cha timu ya Taifa
kinachoingia kambini kesho.
Katika
hatua nyingine Mkwasa ametangaza benchi la ufundi la Taifa Stars, kocha
msaidizi Hemed Morocco, kocha wa magolikipa Peter Manyika, Mshauri wa
timu Abdallah Kibadeni, mtunza vifaa Hussein Swedi Gaga huku mratibu wa
timu akiwa ni Alhaj Ahemd Mgoyi.
Kamati ya tiba ya TFF itapendekeza majina ya daktari wa timu na mchua misuli watakaoungana na kambi ya Taifa Stars.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)


0 comments :
Post a Comment