- Written by Nkupamah Blog
Mwakilishi
wa shirika la WaterAid Tanzania, Ibrahimu Kabole, akitoa ufafanuzi juu
ya mradi wa ‘Mwanzo Mwema’ (A Good Start) ambao pamoja na mambo mengine,
utashughulikia afya ya uzazi kwa akina mama wajawazito. Mradi huo
unafadhiliwa na
serikali ya Sweden.Kulia ni balozi wa Sweden hapa
nchini, Lennarth Hjelmaker.(Picha na Nathaniel Limu).
Na
Nathaniel Limu, SingidaSHIRIKA lisilo la kiserikali la WaterAid
Tanzania,limeahidi kushirikiana na klabu ya waandishi wa habari
(Singpress) mkoa wa Singida, kwenye utekelezaji wa mradi wa ‘Mwanzo
mwema’ (A Good Start) unaodhaminiwa na serikali ya Sweden kupitia
shirika la Riksfӧbundet FӧR Sexual Upplysning (RFSU).Ahadi hiyo
imetolewa na Mwakilishi wa shirika la WaterAid Tanzania Dk.Ibrahimu
Kabole,muda mfupi baada ya mradi wa Mwnzao Mwema utakaogharamu zaidi ya
shilingi 1.4 biloni,kuzinduliwa rasmi mjini hapa na balozi wa Sweden
nchini Lennarth Hjelmaker.Alisema mradi wa Mwanzo Mwema utakaotekelezwa
kwa kipindi cha miaka mitatu katika halmashauri ya wilaya ya Iramba na
manispaa ya Singida,lengo lake ni pamoja na kutoa elimu juu ya uzazi wa
mpango,haki za binadamu na mambo yanayoambatana na uzazi.Dk.Kabole
alisema pia kuwa itatolewa elimu juu ya haki ya wasichana kuamua kuolewa
na vile vile kuhamasisha wasichana ikiwemo wale ambao hawakumaliza
darsa la saba kupata haki yao ya elimu kadri uwezo wao
utakavyowaruhusu.“Vile vile mradi huu, katika kipindi chake cha
utekelezaji,utajikita katika kupunguza/kumaliza kero ya uhaba wa
maji,vitendea kazi na kuboresha usafi wa mazingira katika vituo vya
kutolea huduma ya afya, ili vituo hivyo viwe kimbilio kwa akina mama
wajawazito kujifungulia huko”, alifafanua Dk.Kabole.Mwakilishi huyo
alisema ili malengo ya mradi huo wa aina yake nchini yaweze kufikiwa kwa
wakati uliopangwa,mchango wa waandishi wa habari kupitia taaluma
yao,unahitajika mno.“Waandishi wa habari wakitumia vyema taaluma yao
katika kuandaa vipindi maalumu au kuandika makala kwenye magazeti
mbalimbali kuelimisha na kuhamasisha jamii umuhimu wa afya ya
uzazi,usafi wa mazingira katika maeneo ya vituo vya kutolea huduma ya
afya, wasichana ambao hawajapata elimu waipate haki hiyo,pia wajue kuwa
wana haki ya kuolewa ipo mikononi mwao na haki za binadamu kwa ujumla,
lengo la mradi huu litafikiwa kwa ufanisi mkubwa”,alifafanua
Dk.Kabole.Shirika la WaterAid Tanzania litashirikiana na mashirika
mengine ya SEMA, Amref, RFSU katika kutekeleza mradi huo unaofadhiliwa
na serikali ya Sweden.Sweden pia imekuwa mdau mkubwa katika kuendeleza
tasnia ya habari nchini kwa kipindi kirefu ikishirikiana na Umoja wa
vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC).Ufadhili wa nchi ya
Sweden umekuwa na miradi ya kutoa mafunzo mbalimbali kwa waandishi wa
habari nchini, na kufadhili vyombo mbalimbali vya ofisi mbalimbali kwa
ofisi za vilabu vya waandishi wa habari mikoani.


0 comments :
Post a Comment