Monday, June 29, 2015
Nkupamah blog
Kwa
mara ya kwanza, ‘mnyama’ katika anga la muziki wa Bongo Fleva, Khaleed
Mohamed ‘Top In Dar’ (TID) amekiri kutumia mihadarati aina ya bangi huku
akijiapiza kuwa hajawahi kutumia madawa mengine ya kulevya ‘unga’
ikiwemo cocaine kama ambavyo amekuwa akinyoshewa vidole na baadhi ya
watu.
Akizungumza
na Gazeti la Ijumaa katika mahojiano maalum wikiendi iliyopita, TID
ambaye ni mmiliki wa Top Band alifunguka kuwa miongoni mwa mambo
yanayomkosesha raha na amani ya moyo, ni pamoja na kuhukumiwa
kujihusisha na matumizi ya unga na wengine kwenda mbele kwa kusema hata
kushuka kwake kisanii kumechangiwa na ishu hiyo.
Staa
huyo wa Ngoma ya Kiuno alisema kuwa, wakati mwingine watu wanamsakama
hadi mama yake mzazi wakimtaka amkanye mwanaye kujiepusha na maisha ya
‘kubwia unga’ jambo ambalo linampa wakati mgumu na kujiona kuonewa
katika jamii.
Kuhusu
kushuka kimuziki, TID alisema miongoni mwa sababu zilizosababisha
kuporomoka katika anga la muziki ni kile alichokiita ‘hujuma’ kutoka kwa
baadhi ya wadau wakubwa wa muziki (majina yapo), kwa kushindwa kumpa
fursa za kimuziki zikiwemo promosheni na mialiko ya shoo kwa kuwa wana
vinyongo na fitina dhidi yake.
“Kaka, naonewa kabisa nikihusishwa natumia madawa ya kulevya, wanamsumbua mama eti akae na mimi anionye.
“Jamani situmii madawa ya kulevya kama cocaine, ila kwa upande wa bangi ni sawa nakubali kuwa navuta.
“Lakini
pia, kuvuta kwangu bangi siyo sababu ya mimi kushuka kisanii, zipo
sababu zingine kabisa kama kuhujumiwa na wadau wakubwa wa soko la muziki
kutokana na mabifu yanayotokana na sababu binafsi.
“Hivi
kweli mtu anayetumia madawa ya kulevya kama cocaine, anaweza kumudu
maisha kama kununua nyumba? Kununua magari? Hata kuendelea kuimba kweli?
Siyo sawa jamani,” alisema TID.
Nkupamah blog
0 comments :
Post a Comment