Ugiriki yaidhinisha kura ya maoni
Bunge la
Ugiriki limeidhinisha kura ya maoni iliyokuwa imetishwa na waziri mkuu
wa nchi hiyo Alexis Tsipras kuhusu mpango wa kuisaidia kiuchumi nchi
hiyo uliopendekezwa na wakopeshaji wake.
Akizungumza
kabla ya kura hiyo, bwana Tsipras amewataka watu nchini Ugiriki kupiga
kura ya hapana kwenye kura ambayo itafanyika tarehe 5 mwezi Julai.
Amewalamu
wakopeshaji wa nchi hiyo wakiwemo muungano wa ulaya, benki kuu ya Ulaya
na shirika la fedha duniani kwa kuihangaisha ugiriki.
Amesema kuwa kura ya hapana itaipa ugiriki uwezo wa kufanya majadiliano.BBC
0 comments :
Post a Comment