Saturday, June 27, 2015
Nkupamah blog
MBUNGE
wa Manyoni Mashariki, Kapteni John Chiligati, amesema baadhi ya
wananchi jimboni kwake wameanza kula ubuyu kutokana na kukabiliwa na
tatizo la njaa.
Katika
swali lake bungeni jana, Mbunge huyo alitaka kujua ni lini Serikali
itapeleka chakula cha msaada haraka ili kuwanusuru wananchi hao.
“Lini
Serikali itaanza kugawa chakula cha msaada kwa kuwa jimboni kwangu kuna
uhaba wa chakula, hasa katika maeneo ya Kintiku ambapo baadhi yao
wameanza kula ubuyu?” alisema Kapteni Chiligati.
Akijibu
swali hilo, Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi,
alisema taratibu za kuomba chakula cha msaada zinatakiwa kuanzia
wilayani kwa kufanya tathmini.
“Wilaya
ikishafanya tathmini inatakiwa kuipeleka katika kikao cha Ushauri cha
Mkoa (RCC), RCC itapeleka Ofisi ya Waziri Mkuu ambao wataleta wizarani
kwetu kwa ajili ya kupeleka chakula cha msaada. Chakula kipo cha
kutosha, mikoa husika inatakiwa kufanya tathmini ili ituletee watu
wasije wakafa njaa,” alisema.
Awali
Zambi akijibu swali la msingi la Kapteni Chiligati, lililohoji iwapo
serikali ipo tayari kushirikiana na wananchi wa Manyoni kupitia
Halmashauri ya wilaya hiyo kuhakikisha ujenzi wa bwawa la Mbwasa
unakamilika, alisema ujenzi huo utafanyika pamoja na skimu ya
umwagiliaji ya Mwiboo.
“Skimu
ya Mwiboo haipo katika skimu 78 zinazotekelezwa kupitia Mpango wa
Matokeo Makubwa Sasa (BRN). Wizara kwa kushirikiana na halmashauri za
wilaya zimeandaa andiko kwa ajili ya kuomba fedha kwa washirika wa
maendeleo ambao maombi ya Sh milioni 400 yamewasilishwa,” alisema Zambi.
Nkupamah blog
0 comments :
Post a Comment