Na Andrew Chale, modewjiblog
(Dar
Es Salaam) Shirika la ndege la Fastjet limeendelea kupanua wigo wake
kwa kuanzisha safari zaidi ikiwa ni kuunganisha Afrika kuwa moja kupitia
safari za anga kwa gharama nafuu kabisa ambapo asubuhi ya leo
wanatarajia kuizindua rasmi ‘route’ hiyo ambayo inakuwa ni ya tano ya
kutoka Dar es Salaam-Tanznaia kwenda Lilongwe-Malawi.
Awali
akielezea kwa wandishi wa habari, Meneja Mkuu wa shirika la Ndege la
Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati alipokutana Zanzibar wakati wa
tamasha la 18, la filamu za nchi za Majahazi maarufu ZIFF ambapo pia
Fastjet ni wa zamani kwa mwaka wa pili mfululizo, alibainisha kuwa maar
azote shirika hilo linakuja na huduma bora na kwa gharama nafuu
kumsaidia mteja kufanikisha mambo yake mbalimbali kupitia usafiri wa
anga.
Anasema
kuanzishwa kwa ‘route’ hiyo ya Lilongwe (Malawi), fastjet ipo pia
mbioni kufikia nchi zingine ndani ya Afrika na kwa sasa ipo katika
mchakato huo na baadae wataweza kutangaza rasmi huku akiwataka wateja
kujitokeza kwa wingi kuwaunga mkono katika juhudi hizo za usafirishaji
wa anga.
“Tunajisikia
furaha kuweza kusogeza huduma zaidi wateja waliokuwa wakitumia muda
mrefu kusafiri kutumia usafiri mwingine kuelekea Malawi, sasa wamepata
mkombozi Fastjet ambayo itakuwa ikiruka mara mbili kwa wiki Jumatatu na
Ijumaa!… kwa gharama nafuu kabisa” alieleza Kibati.
Kwa
upande wake, Afisa Mahusiano na Masoko wa Fastjet, Lucy Mbogoro
anasema tayari watu mbalimbali wameweza kuchangamkia ‘route’ hiyo ya
kuelekea Malawi kwani itaendelea kuunganisha watu wote karibu huku
ikitoa fursa kwa wafanyabiashara, wanafunzi, shughuli za kiserikali,
michezo pamoja na zingine nyingi ikiwemo za kifamilia.
Awali
Fastjet ilianzia na safari za ndani za kusafirisha abiria ‘route’ za
Mwanza – Dar, Kilimanjaro – Dar na Mbeya – Dar na baadae kuweza kuvuka
mipaka zaidi kwa nchi za Afrika kwa ‘rout’ kati ya Dar – Johannesburg
(Afrika Kusini), Dar – Lusaka (Zambia), Dar – Harare (Zimbabwe), Dar –
Entebbe (Uganda) na kwa sasa hii inayozinduliwa leo Julai 27, ya
Dar-Lilongwe (Malawi).
Afisa
huyo, anaeleza kuwa, Fastjet itaendelea kutoa huduma bora kupitia
usafiri wa anga huku akisisitiza kuwa ‘route’ mbalimbali zikiwa mbioni
kufikiwa na shirika hilo.
Want to take your business to Malawi’s thriving capital city?
Now
you can. Our new international route connects Lilongwe with Dar es
Salaam every Monday and Friday with fares available from just Tsh
237,600/$99 (Tsh 120,000/$50 fare, plus Tsh 117,600 tax/$49 gov.taxes).
Tickets
are on sale now with flights departing from 27th July, so save yourself
the hassle of a long drive and fly further for less with fastjet.com


0 comments :
Post a Comment