Homa
ya michuano ya Kagame inazidi kupamba moto kufuatia vilabu mbalimbali
zinazoshirki michuano hiyo kuanza kuwasili jijini Dar es salaam zikiwa
na vikosi vyao kamili kwa lengo la kusaka Ubingwa wa michuano hiyo.
APR ya
Rwanda tayari imeshawasili jijjini Dar es salaam, pamoja na timu za Al
Shandy ya Sudan, KMKM ya Visiwani Znzibar, huku timu za Al Malakia ya
Sudan Kusini na mabingwa mara tano wa michuano hiyo Gor Mahia
wakitarajiwa kuwasili leo saa saa 10 jioni kwa ndege ya Kenya (KQ).
Kueleka
mchezo wa ufunguzi kati ya Yanga dhidi ya Gor Mahia, wenyeji timu ya
Yanga (watoto wa Jangwani) wameendelea kujifua katika uwanja wa Polisi
Ufundi chini ya kocha wake mholanzi Hans Van der Pluijm na msaidizi wake
Mkwasa kuhakikisha wanafanya vizuri katika mechi hiyo.
Gor
Mahia ambayo inafundishwa na kocha Frank Nutal raia Skotilandi,
inawasili ikiwa na kikosi chake cha kwanza kamili kilichocheza michezo
17 ya Ligi Kuu nchini Kenya bila kufungwa, ikishinda michezo minne na
sare michezo mitatu.
Wasifu wa Azam:
Klabu
ya Azam ilishiriki kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya kombe la Kagame
mwaka 2012 lakini walishangaza wengi kwa kumaliza kama washindi wa pili
baada ya kufungwa na Yanga mabao 2-0 kwenye mchezo wa fainali.
Mwaka jana ilishiriki kwa mara ya pili na kuishia hatua ya robo fainali baada ya kutolewa na Al Merriekh kwa mikwaju ya penati.
Kundi ililopo:
Azam
iko kwenye kundi C ikijumuishwa na KCCA ya Uganda, Adama City ya
Ethiopia na, Azam inapewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri mwaka huu
ikiundwa na wachezaji wengi waliokaa pamoja kwa muda mrefu.
Wachezaji wa kuangaliwa.
Kwa upande wa ushambuliaji inawategemea wachezaji kama Kipre Tchetche, Didier Kavumbagu.
Nahodha
mzoefu wa Azam, John Bocco bado anaweza kuwa na mchango mkubwa. Mlinzi
mahiri, Pascal Wawa anatarajiwa kuhakikisha ngome ya Azam haipitiki kwa
urahisi. Brian Majwega, Salum Abubakar na Michel Bolou ni wachezaji
wengine ambao ni nyota na muhimu kwenye timu hii.
Benchi la Ufundi:
Benchi
la ufundi la Azam lipo chini ya usimamizi wa kocha Muingereza, Stewart
Hall. Ni mara ya tatu kwa kocha Stewart Hall kuifundisha Azam.
Bila
shaka, kocha Hall atakuwa na malengo ya kupiga hatua moja Zaidi baada
ya kukaribia kubeba taji la Kombe la Kagame miaka mitatu iliyopita.
Rekodi Kombe la Kagame:
Azam
inashiriki Kombe la Kagame kwa mara ya tatu. Mafanikio yake makubwa ni
kufika fainali mnamo mwaka 2012 ilipolazwa mabao 2-0 na Yanga.
Wasifu wa KCCA:
Klabu
hii inayomilikiwa na halmashauri ya jiji la Kampala ni moja ya timu
kubwa Uganda ikichuana na timu maarufu Zaidi nchini humo, SC Villa na
Express.
Wakati
vigogo Sc Villa na Express wakionekana kusuasua, KCCA imeendelea kutoa
makucha kwenye ligi ya Uganda licha ya kupoteza ubingwa wao msimu
uliopita.
KCCA
iliyowahi kufundishwa na Kocha msaidizi wa Azam, George Nsimbe inasifika
kwa kucheza soka la kasi, ikishambulia Zaidi kutokea pembeni.
Baada
ya kupoteza ubingwa walioshikilia mara mbili mfululizo, KCCA imejipanga
upya kwa kusajili wachezaji wapya 11 na kutema idadi kama hio ya
wachezaji walionekana kuwa mzigo.
Kundi Ililopo:
KCCA
iko Kundi pamoja na Azam, Adama City ya Ethiopia, Malakia ya Sudani
Kusini. Itakuwa miujiza KCCA kushindwa kufuzu kwa hatua ya robo fainali
kutoka kundi hili.
Wachezaji wa kuangaliwa:
Tom
Masiko ni kati ya viungo wanaotarajiwa kung’ara kwenye Kombe la Kagame.
Walinzi Saka Mpima na Habib Kavuma ni kati ya walinzi wanaosifika kwa
kushambulia licha licha ya kuwa kazi ya kulinda lango lao.
Mtanzania,
Shaban Kondo aliyesajiliwa kwa ajili ya msimu huu mpya, anatarajiwa
kuwa moja ya mchezaji atakayetazamwa kuona nini miguu yake inaweza
kufanya akiwa dimbani.
Benchi la ufundi:
KCCA
wanaonekana kuwa na benchi la ufundi pana Zaidi kuliko timu nyingi
kwenye mashindano yam waka huu. Benchi lao la ufundi linajumuisha
makocha saba chini ya usimamizi mkuu wa Mike Mutebi akisaidiwa na kocha
Sam Ssimbwa
Rekodi Kombe la Kagame:
Ni
mabingwa mara moja wa michuano hii wakiwa wamebeba kombe hilo mwaka
1978. Mwaka walifika katika hatua ya fainali lakini hawakubahati kupata
ushindi mbele ya Al Merriekh ya Sudani.
NB:
Kesho siku ya ijuma saa 5 kamili asubuhi, kutakua na mkutano na
waandishi wa habari katika ukumbi wa TFF uliopo Karume. Rais wa CECAFA,
Rais wa TFF na makatibu wakuu wa TFF na CECAFA watakuwepo.
Waandishi wa habari mnaombwa kuhudhuria bila kukosa.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)



0 comments :
Post a Comment