@nkupamah blog
Mmoja wa wagombea wa Ubunge Jimbo
la Iramba, Mkoani Singida Davd Jairo akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani, juu ya madai yao ya kugomea kuendelea na mchakato wa
kura za maoni hadi msimamizi wa uchaguzi ambae ni katibu wa CCM Wilaya
ya Iramba Mathias Shidagisha aondolewe kwenye zoezi hilo, kulia ni David
Jairo na kushoto ni Amon Gyunda .
Mmoja wa wagombea wa Ubunge Jimbo
la Iramba, Mkoani Singida Juma Killimbah akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani) kwenye ofisi za chama cha waandishi wa habari
Mkoani humo Singpress.
Kilimbah akionesha waandishi mojawapo ya sms za M pesa zlizotumwa na Mwigulu kwa Mmoja wa wapiga kura ili kumchagua yeye.
…………………………………………………………..
Na Hillary Shoo, KIOMBOI.
WAKATI zoezi la wagombea Ubunge
kujinadi na kuomba kura kwa wananchi likiendele kote nchini ,hali sio
shwari ndani ya CCM Wilaya ya Iramba, baada ya wagombea watatu kati ya
wanne kutangaza kugomea mchakato wa kura za maoni kwa madai kuwa Katibu
wa CCM Wilaya ya Iramba anambeba waziwazi mgombea mwezao Mwigulu
Nchemba.
Wakizungumza na waandishi wa
habari jana na kutoa tamko kwa chama Mkoa wagombea hao, David
Jairo, Juma Killimbah na Amon Gyunda wamesema kuwa wameamua kuchukua
hatua hiyo kutokana na msimamizi wa uchaguzi kura za maoni katika jimbo
hilo, ambaye ni Katibu wa CCM Wilaya ya Iramba, Mathias Shidagisha na
msaidizi wake, Mwita Raphael, kuwachezea rafu mbaya.
Jumba Killimbah alidai kuwa
mgombea mwenzao Mwigulu Nchemba amekuwa akivunja kwa makusudi kanuni na
taratibu za mchakato wa uchaguzi huo huku viongozi wa kamati ya Siasa
wakifumbua macho hali hiyo.
“Kanuni za uteuzi wa wagombea wa
CCM kuingia katika vyombo vya dola toleo la Feb 2010, fungu la 3 kanuni
ya 17 (v) (1) kimeeleza bayana namna ya kura ya maoni na mikutano mikuu
ya kampeni ya matawi itakavyotendeka ambapo inasisitiza wahusika ni
wanachama tu.” .Alisema na kuongeza;
“Lakini kwa utaratibu usio rasmi,
mikutano hiyo jimboni kwetu ni ya hadhara isiyozingatia akidi ya
wanachama na kunakuwepo na wanachama kutoka vyama pinzani ambao
hushiriki kikamilifu kuuliza maswali kwa wagombea”.
Aidha, alidai kuwa msimamizi huyo
amekuwa akitumia gari la Mwigulu kusambaza mabango yake hadharani kwenye
kata mbali mbali huku akitoa maelekezo kwa makatibu wote wa matawi
kuhakikisha Mwigulu anashinda.
“Pia amekuwa akimruhusu mgombea
huyo kuambatana na magari yasiopungua 10, pikipiki 100, baiskeli zisizo
na idadi na kuhama na wapambe wake kila eneo la mkutano huku akitumia
gari kubwa lenye vipaza sauti” alisema Killimbah.
Aidha alidai kuwa Shidagisha
amekuwa akidiriki kubariki matusi wanayotukanwa na mgombea mwenzao
Mwigulu licha ya kulalamika mra kwa mara lakini Katibu huyo amekuwa
akiwataka watwangane wawezavyo mbele ya wapiga kura wao.
Hata hivyo walidai kuwa Mwigulu
amekuwa akitumia gari ya umma wa Wizara ya fedha yenye namba za usajili
STL 3400 aina ya Land cruiser, gari ambalo alitumia siku ya kuchukua
fomu likiwa na namba NW FH.
“Kwa kuwa ni dhahiri msimamizi
huyu hawezi kutenda haki na hasa ya kusimamia matokeo ya uchaguzi na kwa
kuwa ameshatamka bayana tena kwa viapo na huku akitishia kuwapiga
baadhi ya wagombea , sisi kama wagombea tumeonelea tumkatae ndugu
Shidagisha na msaidizi wake Mwita Rafael kuendelea kuwa wasimamizi wa
uchaguzi Jiimbo la Iramba, sambamba na kuchukuliwa hatua za akimaadili
na pia Katibu wa UVCCM Wilaya Abel Makala kuacha kuwa kampeni meneja wa
Mwigulu huku akitumia wadhifa wake.” Alifafanunua Jairo.
Hata hivyo Killimbah alionesha
waandishi wa habari sms inayoonesha kuwa Mwigulu alimtumia mmoja wa
wajumbe fedha kiasi cha shilingi laki moja kama njia mojawapo ya
kumshawishi kumpigia kura.
Akizungumzia malalamiko ya
wagombea hao,Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Aluu Segamba alisema
ni kweli yapo na kwamba sekretarieti ya mkoa ilitarajiwa kwenda
Wilayani Iramba jana kushughulikia suala hilo.
“Hizi ni changamoto za uchaguzi
na hawa ni watu wazima, ni imani yangu tutafikia muafaka maana tutawaita
wagombea wote pamoja na kamati ya Siasa ya Wilaya ili tumalize tatizo
hili haraka iwezekanavyo.”. Alisema Segamba.
0 comments :
Post a Comment