Wednesday, July 15, 2015
Nkupamahmedia blog
Mwanasiasa Mkongwe katika medani za siasa nchini Tanzania ameibuka na kuzungumza na Waandishi wa Habari leo kuhusiana na mchakato wa kumpata mgombea Urais CCM uliopelekea jina la Mbunge wa Monduli Edward Lowassa kukatwa.
Akizungumza
katika mkutano huo Kingunge amesema Kamati ya Maadili huko nyuma
ilikuwa ni chombo cha kuandaa taarifa ili kuisadia Kamati Kuu katika
kuwajadili wagombea lakini safari hii Kamati ya Maadili imefanya kazi
isiyowahusu kikatiba ikiwemo kukata majina ya wagombea.
Amesema
Kamati ya Maadili ya Chama cha Mapinduzi (CCM) yenyewe imekosa maadili
ya kuheshimu katiba na taratibu za chama kwa kujipa madaraka ya
kupeleka majina 5 kwenye kamati kuu, ambayo ilipaswa kuhoji wagombea
wote 38.
“Kuna baadhi ya watu waliamua kuitumia Kamati ya Maadili kuandaa watu wao na kuwakata wengine kwa sababu zao.” Amesema Kingunge.
Kingunge
amedai kwamba CCM ni chama cha wanachama wote, taratibu na kanuni
zikipuuzwa na kufanya vitu kwa maamuzi ya kikundi fulani, amedai kuwa
kwenye vikao vya CCM Ulifanyika uhuni na dharau kwa wanachama wengine.
"Wakubwa waliopewa madaraka wanaona hakuna lolote tunaloweza kufanya."
"Wakubwa waliopewa madaraka wanaona hakuna lolote tunaloweza kufanya."
Amesisitiza
kuwa kilichofanyika Dodoma hakikuwa sawa, Kamati Kuu iliporwa kazi
yake, hii ni dharau kwa wanachama na wagombea wote. Kamati Kuu ya Taifa
CCM, ipo chini ya Halmshauri Kuu ya Taifa yenye madaraka ya kujadili
mapendekezo yalioletwa na Kamati Kuu, na Halmshauri Kuu ina madaraka ya
kukataa au kukubali mapendekezo yalioletwa na Kamati Kuu, lakini
utaratibu huo haukuwepo
Kingunge
amesema anawaheshimu sana Mzee Benjamin Mkapa, Mwinyi, na Karume,
lakini amesikitika kuwa ndio waliotoa michango ya kutotoa haki
kwenye Kamati Kuu.
"Waliogombea 1995 walikuwa 16, Kamati Kuu iliwasikiliza na kuandaa orodha ya watu 6,” alisema Kingunge.
"Waliogombea 1995 walikuwa 16, Kamati Kuu iliwasikiliza na kuandaa orodha ya watu 6,” alisema Kingunge.
Akizungumzia
yaliyokea NEC Kingunge amesema wajumbe walihoji kwa nini Jina La
Lowassa halikuwemo, mjadala ulikuwa mgumu, watu walisema lazima aingie
kwenye orodha. "......Kwa mara ya kwanza muundo wa Chama ulijaribiwa baada ya wajumbe kutaka jina la Lowassa kwenye orodha ya majina 5."
Kwa
upande mwingine, amewapongeza wajumbe walijitokeza kukataa maamuzi ya
Kamati Kuu ikiwemo Adam Kimbisa, Mbunge wa Songea Emmanuel Nchimbi na
Sophia Simba.
Akizungumzia kauli ya Mbunge huyo kuhusishwa na ufisadi Kingunge amesema,
"Hadithi
ya Lowassa kuwa ni fisadi haina mashiko, ilianza kwa kashfa ya
Richmond. Kamati teule ya Bunge iliundwa na kutoa taarifa za ovyo sana,
na hatimaye kwa kulinda heshima ya serikali na chama akajiuzulu."
Kingunge
ameongeza kuwa Lowassa sio wa kwanza kuwajibika kisiasa .Amesema
katika awamu ya kwanza ya Mwalimu –walikuwemo viongozi wa kisiasa
waliouzulu.
Amewataja waliowahi kujiuzulu kuwa ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Ali Hassani Mwinyi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na Mkurugenzi wa Usalama Taifa wote walijiuzulu kisiasa na Mwalimu aliwashukuru kwa kuwajibika.
Amewataja waliowahi kujiuzulu kuwa ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Ali Hassani Mwinyi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na Mkurugenzi wa Usalama Taifa wote walijiuzulu kisiasa na Mwalimu aliwashukuru kwa kuwajibika.
“Lowassa
alijiuzulu kuwajibika kisiasa, lakini ikabadilishwa kuonekana ni yeye
ndiye aliyefanya makosa, ndio ukaanza wimbo wa ufisadi. Serikali yenyewe
ilimsafisha kupitia TAKUKURU, lakini wimbo wa ufisadi ukaendelea,
wakaja na wimbo mwingine wa Gamba.
“Yote haya yalipangwa na ‘Kitengo’ kilichoandaa kashfa ya Richmond. Edward ana historia ndefu ndani ya Chama.” amesema mzee Kingunge.
Amesisitiza
kuwa Uongozi wa Chama na Nchi umetumia nguvu kubwa sana kupuuza
wananchi wanataka nini na kuhakikisha wanayempenda hapati kitu
Ametumia
mkutano huo pia kuwaomba viongozi ndani ya CCM warudi kusoma ahadi za
mwanachama, warudi pia wasome utangulizi wa katiba ya CCM na kusisitiza
kuwa kilichotokea Dodoma hakikubaliki, si halali na si haki.
Nkupamahmedia blog



0 comments :
Post a Comment