
Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Diaspora kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa Bi. Rosemary Jairo akiongea na waandishi wa
Habari kuhusu Maandalizi ya Kongamano la Diaspora (Tanzania and SMEs
Partnership Conference 2015) litakalofanyika kuanzia tarehe 13-15 Agosti
2015 Jijini
Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya
Habari (MAELEZO), Leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya
waandishi wa Habari wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Idara ya Diaspora
kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bi. Rosemary
Jairo.Picha na Hassan Silayo-MAELEZO.(VICTOR)
Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha
Uwekezaji cha Kimataifa (International Trade Centre UN-Agency) inafanya
Maandalizi ya Kongamano la Diaspora (Tanzania Diaspora & SMEs
Partnership Conference 2015). Kongamano husika litafanyika hapa Dar es
Salaam, kuanzia tarehe 13 hadi 15 Agosti 2015 katika Hoteli ya Serena.
Kongamano hilo litakuwa la pili kufanyika hapa nchini na litahusisha
Diaspora na Wadau wa hapa Tanzania.
Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ofisi ya Rais na Utawala Bora
– Zanzibar na Ofisi ya Waziri Mkuu ndio Wadau Wakuu katika Maandalizi
ya Kongamano hili. Kongamano la mwaka huu lina Kauli Mbiu, ‘Creating
Linkages between Diaspora and Local SMEs in Tanzania’ na Dhumuni lake ni
kuhamasisha Ushiriki wa Diaspora katika kukuza Biashara Ndogo na za
Kati hapa nchini. Kongamano la mwaka huu pia litahusisha Mikoa ya
Tanzania ambapo Mikoa itapata fursa ya kutangaza fursa za uwekezaji
zilizopo Mikoani.
Kongamano
hilo linatarajiwa kufunguliwa na Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kufungwa na Mhe. Dr. Ali Mohamed
Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Aidha,
katika kuhitimisha kilele cha Kongamano hilo, Diaspora wanatarajiwa
kufanya ziara Zanzibar tarehe 15 Agosti 2015, ikiwa ni sehemu ya mwaliko
maalum kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Pamoja na
Shughuli za Ufunguzi na Kilele, Matukio muhimu yatakuwa ni Maonesho ya
Kibiashara, Majadiliano ya Mada kuhusu Ushirikishwaji wa Diaspora kwa
Maendeleo ya Nchi hususan SMEs, uwekezaji Mikoani n.k.
Kongamano
hilo litahudhuriwa na Watanzania Wanaoishi Ughaibuni (Diaspora) na wale
waliorejea hapa nchini na Wadau wa Maendeleo kutoka hapa nchini.
Wizara ya
Mambo ya Nje inawakaribisha kushiriki nasi katika Kongamano hilo.
Tafadhali tembeleeni tovuti ya (www.tzdiaspora.com) kupata taarifa
muhimu hususan kuhusu Ada za Ushiriki, fursa za Kufadhili na namna ya
kujisajili.
Imetolewa na: Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dar es Salaam 21 Julai, 2015


0 comments :
Post a Comment