Waziri
wa Ujenzi nchini Tanzania, John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni
rasmi katika ufunguzi wa michuano ya Kombe la Kagame siku ya Jumamosi,
Julai 18 2015 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Magufuli
baada ya kufungua rasmi michuano hiyo, atashuhudia mchezo wa ufunguzi
rasmi wa mashindano ya Kagame, mechi itakayowakutanisha miamba ya Afrika
Mashariki timu ya Yanga dhidi ya Gor Mahia kutoka nchini Kenya.
Michuano
ya Kagame inatarajiwa kuanza kutimua vumbi siku ya jumamosi kwa michezo
mitatu, ukindoa mecho ya Yanga Vs Gor Mahia, mechi zingine zitakua ni
kati ya APR dhidi ya Al Shandy uwanja wa Taifa saa 8 mchana, KMKM Vs
Telecom saa 10 jioni uwanja wa Karume.
Kuanzia leo tutakua tunawaleta kwa ufupi timu zinazoshiriki michuano hiyo mwaka huu, na kwa kuanza tunaanza na kundi A;
Mchezo
wa ufunguzi kati ya Yanga dhidi ya Gor Mahia unaonekana kuteka hisia
za wapenzi wa soka kwa ukanda wa Afrika Mashariki, kwani ni takribani
miaka 19 timu hizo mbili haziwaji kukutana katika ardhi ya Tanzania.
Mara
ya mwisho mwaka 1996 katika michuano ya Cecafa, timu hizo zilikuwa
katika kundi moja, katika mchezo wa awali zilitoka sare ya bao 1- 1,
wakati zilipokutana katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu, Gor Mahia
iliibuka na ushindi wa mabao 4 -0.
Gumzo
la wadau wa soka nchini kwa sasa ni kuhusu uwezo wa klabu za Tanzania,
Yanga, Azam na KMKM kuweza kuhakikisha kombe la michuano ya Klabu Bingwa
Afrika Mashariki haliondoki kwenye ardhi ya
Tanzania.
Kwa
upande wa Yanga, matumaini ya kulibakiza kombe kwenye ardhi ya Tanzania
yatachagizwa na historia yao nzuri ya miaka ya hivi karibuni pindi Kombe
la Kagame linapoandaliwa nchini. Yanga iliibuka kidedea mara mbili
mfululizo mwaka 2011 na 2012 mashindano hayo yalipoandaliwa nchini.
Yanga
mabingwa mara tano wa michuano hio watakuwa na kazi moja tu ya kujaribu
kuifikia rekodi ya Simba, inayoongoza kutwaa Kombe hilo mara nyingi,
ikiwa imeweza kufanya hivyo, mara sita.
Kocha: Hans van Pluijm ( Uholanzi)
Yanga iko chini ya mtaalam kutoka Uholanzi, Hans van Pluijm anayesifika kwa kuwa mfuasi asiyetetereka wa soka la kushambulia.
Nyota wa kutazamwa:
Yanga
ina wachezaji kadhaa inaowategemea ili kufanya vizuri. Macho na masikio
yataelekezwa kwa Donald Ngoma, mshambuliaji aliyesainiwa kutoka
Platinum Fc ya Zimbabwe kuona kama ataendeleza kasi yake ya ufungaji
aliyoanza nayo.
Haruna
Niyonzima, Simon Msuva, Nadir Haroub na Amissi Tambwe ni kati ya
wachezaji ambao wanatarajiwa kuendelea kuwa nguzo za Yanga kwenye
michuano hii.
Rekodi kwenye Kombe la Klabu Bingwa:
Yanga imebahatika kutwaa ubingwa mara tano; (Mwaka 1975, 1993, 1999, 2011, na 2012).
Pia
Yanga imemaliza kama washindi wa pili mara mbili, mwaka 1976 ilipofungwa
na Gor Mahia 2-1 jijini Kampala na mwaka 1992 ilipolala kwa mikwaju ya
penati mbele ya watani wao wa jadi, Simba.
Kuanzishwa:
Yanga ilianzishwa mwaka 1935, na kuwa moja ya klabu kongwe kabisa kwenye ukanda huu na bara la Afrika kwa ujumla.
Gor Mahia: Wababe wa Kenya waliojipanga upya kurudisha heshima.
Gor Mahia hawakufanya vizuri katika michuano ya mwaka jana, ila wanatarajiwa kutoa ushindani katika mashindano ya mwaka huu.
Licha
ya kupotea kwa muda mrefu kabla ya kuibuka na kushindwa kufurukuta
kwenye michauno ya mwaka jana jijini Kigali, Gor Mahia wanajipa moyo
Zaidi kutokana na mwenendo wao kwenye Ligi ya
Kenya.
Mabingwa hao wa Kenya hawajapoteza mechi msimu huu huku wakionesha dalili za kutangaza ubingwa mapema kabisa.
Kundi lake:
Gor Mahia iko kwenye kundi A la michuano ya mwaka huu ikijumuishwa na Yanga, Al Khartoum ya
Sudan,
KMKM ya Zanzibar na Telecom ya Djibout. Ni kundi ambalo ni gumzo kuu
likdaiwa kuwa na mechi zenye msisimko Zaidi na ushindani mkubwa.
Wachezaji wa kuangaliwa:
Kwa wafuatiliaji wa soka nchini Kenya, hakuna anayepinga kuwa kwa sasa timu yenye wachezaji bora zaidi ni Gor Mahia.
Wachezaji
kama Khalid Aucho, chipukizi Micheal Olunga anayetajwa kuwa mrithi wa
mshambuliaji bora kuwahi kutokea nchini Kenya, Dennis Oliech, na Meddie
Kagere wamekuwa ni kiungo muhimu kwenye timu hii.
Wachezaji wengine ni pamoja na mlinda mlango Boniface Oluoch zake kutikiswa kwenye ligi ya Kenya inayoendelea kwa sasa.
Mlinzi wa Uganda Cranes, Godfrey Walusimbi na George Odhiambo wakiongeza chachu kwenye timu hiyo.
Benchi la Ufundi:
Gor
Mahia inaongozwa na kocha Frank Nuttal, raia wa Uskochi. Benchi lao la
ufundi linajumuisha pia mlinda mlango wa zamani wa kimataifa wa Harambe
Stars, Mathew Ottamax ambaye ana jukumu la kuwanoa walinda mlango,
Boniface Oluoch na Jerim Onyango.
Rekodi Kombe la Kagame:
Mara
ya mwisho Gor Mahia ilitwaa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati mwaka
1985, lakini imetwaa ubingwa huo mara 5 (1976, 1977, 1980, 1981, 1985).



0 comments :
Post a Comment