Mix
Gazeti la
Jambo leo limeripoti kuwa Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia,
watoto na wazee, Ummy Mwalimu amesema utafiti unaonesha kuwa kwa kila
watu wanne duniani , mmoja ana matatizo ya afya ya akili.
Kwa mujibu
wa Waziri Ummy wananchi wanapaswa kuwa makini kuchunguza afya zao za
akili kwa sababu utafiti wa shirika la afya duniani ‘WHO’ zinaashiria
kuwa jamii kwa sasa inakumbwa na maradhi mengi ya namna hiyo, Waziri
Ummy alibainisha
>>>’Miongoni
mwa watu wanaopata matatatizo ya kiakili ni wachache tu ambao wanaweza
kufikia na kupata huduma ya afya ya akili, hata hao wanohudhuria vituo
vya afya, ni wachache wamekuwa wakipata huduma stahiki’
Alifafanua sababu za kijamii zinazoweza kusababisha mtu kupata magonjwa ya akili ni umaskini uliokithiri, kutengwa na kubaguliwa na jamii. sababu nyingine alizitaja kuwa ni kunyanyaswa kimwili na kingono, kuwa tegemezi, kupoteza mali, kazi, ulevi, kukosa huduma muhimu na unyanyapaa.
Source: Jambo Leo


0 comments :
Post a Comment