MAHAKAMA YA WILAYA IRINGA MJINI YAAMUA UCHAGUZI WA MITAA 13 URUDIWE MANISPAA YA IRINGA

Mahakama ya Wilaya ya Iringa imetoa hukumu ya kutengua matokeo ya mitaa 13 kutoka Manispaa ya Iringa ili kufanya uchaguzi wa marudio wa Serikali za Mitaa kutokana na kasoro kadhaa zilizojitokeza katika uchaguzi uliofanyika Desemba 14 mwaka 2014.

Hukumu hiyo ilitolewa jana mbele ya mahakamu wakazi wanne ambao ni Andrew Scout, John Mpitanjia, E. Nassoro na Isaya, waliokuwa wanaendesha kesi hizo katika Mahakama ya Wazi ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Iringa.

Chama cha Mapindizi (CCM) kulifungua kesi 35 za madai za uchaguzi wa serikali za mitaa tarehe 13.01.2015 na kuwakilishwa na wakili msomi, Gaster Likatage Mdegela dhidi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na chama wananchi CUF, ambapo kesi 34 zilikuwa za Chadema na kesi moja tu ndio ilikuwa ya CUF.

Aidha, katika kesi hizo mlalamikiwa namba moja alikuwa ni Chadema walioshinda uchaguzi wa serikali za mitaa na mlalamikiwa wa pili alikuwa ni msimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa.

Katika upande utetezi mawakili nane walisimamia kesi hizo ambao ni Barnabas Nyulusi, Mariam Mbano, Leah Francis, Queen Mtove, Catherine Chalwa, Charles Lawisso, Collins Malekela na Jane Massey.

Moja ya kasoro hizo zilizolalamikwa ni kuchanganywa kwa majina ya wagombea wa uenyekiti. 

Hata hivyo, mitaa iliyotenguliwa matokeo yake ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Desemba 14, 2014 kutokana kasoro mbalimbali ni pamoja na SabaSaba Kata ya Gangilonga, Darajani na Kondoa Kata ya Mivinjeni, Ndiuka ‘D’ Kata ya Igumbulo, Kaduma Kata ya Mkimbizi na Semtema ‘A’ Kata ya Kihesa, 

Mitaa mingine ni Nyamhanga ‘B’ Kata ya Kitwiru, Muungano ‘A’na ‘B’ Kata ya Kwakilosa, Kajificheni Kata ya Ilala, Kihodombi ‘B’ Kata Isakalilo, Dodoma Road na Mkimbizi ‘B’ Kata ya Mkimbizi.

Aidha, mahakimu wakazi hao watengua matokeo ya mitaa 13 ili uchaguzi kurudiwa ndani ya siku 30 bila kulipa gharama zozote za uendeshaji wa kesi kwa pande zote mbili za mlalamikaji na mlalamikiwa na rufaa iko wazi.

Awali, Chadema walipeleka mapingazi ya awali 35 mahakamani ili kesi zifutwe kwa gharama lakini kesi nane madai zilitupiwa mbali kwa gharama katika hukumu ndogo (ruling).

Mahakama hiyo ilitupilia mbali kesi nane hizo kwa kukosa ushahidi kwa upande wa mlalalmikaji (CCM).

Kwa mantiki hiyo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimegaragazwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kesi ya msingi ya madai ambapo mahakama ilitenguliwa matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa ili uchaguzi urudiwe katika nafasi ya wenyeviti.

Katika hukumu hiyo ambayo ilitolewa na Mahakama ya Wilaya ya Iringa Juni 30, mwaka huu imekubaliana na hoja za walalamikaji ambao ni wagombea wa CCM washinda mitaa 13 na Chadema wao walishinda mitaa sita katika ya jumla kesi 19 zilizosikilizwa.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment