Afisa
Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama Shekha Nasser Akitoa Mada
kwenye Mradi wake aliouanzisha kuwejengea Uwezo wanawake Kwenye
Ujasiriamali.Mafunzo hayo yalianza jana Chini ya Taasisi ya Manjano
Foundation.Lengo la Mradi huo ni kuwajengea Uwezo wanwake wa Kitanzania
Kupitia Bidhaa bidhaa za Vipodozi vya Luv touch Manjano kujisimamia na
Kujikita Vizuri kwenye Biashara ya Vipodozi na kujua Mbinu Mbalimbali za
Biashara kwa lengo la Kumjengea uwezo Mwanamke wa Kitanzania.
Washiriki
wa Mafunzo ya Usajiriliamali yalio chini ya Manjano Foundation
wakisiliza kwa Makini Mada Mbalimbali kihusu Mafunzo hayo ya kuwajengea
wanawake wa Kitanzania uwezo wa Kudhubutu Kufanya biashara ,Kujisimamia
na Kujua Mbinu Mbalimbali za Biashara Hususani Kupitia Bidhaa za
Vipodozi vya Luv Touch Manjano.
Washiriki wa Wafunzo hayo wakisikiliza kwa Makini.(P.T)
Taasisi
ya Manjano Foundation, ambayo imeanzisha jukwaa kwa ajili ya kuandaa
miradi na programu ambazo zitamuinua mwanamke wa Kitanzania kwa
kumwondolea umasikini wa kipato na ambayo itakuwa ni chachu ya kubadili
yale yote yaliyoyazunguka maisha yake. Taasisi hii limekwishazindua
mradi wenye kubeba bendera yake, Manjano Dream-Makers, mradi unaokusudia
kuzaa kizazi kipya cha wajasiriamali wanawake kwa kutumia kipodozi cha
LuvTouch Manjano tu.
Mradi
huu Uzinduliwa Na Mama Tunu Pinda Ambapo Alisema amefurahishwa sana
Kwa Mwanamke wa Kitanzania Kuzindua Mradi utakaomkomboa Mwanamke wa
Kitanzania Kuondokana na Umaskini kwa Kudhubutu Kujikita kwenye Biashara
hasa kwenye Bidhaa za Vipodozi
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama Shekha Nasser Akiwaeleza jambo washiriki wa Mafunzo hayo..
0 comments :
Post a Comment