Mchuuzi
wa dagaa kwenye mwalo wa Mwigobero uliopo Manispaa ya Musoma, Agnes
Methew, ameibuka mshindi wa kwanza kwenye kura za maoni za kutafuta
Mbunge wa viti maalumu (CCM) mkoa wa Mara.
Akitoa
shukrani kwa wajumbe wa mkutano wa uchaguzi mara baada ya kutangazwa
mshindi na msimamizi wa uchaguzi huo,Samwer Kiboye ambaye ni Mwenyekiti
wa CCM wilaya ya Rorya,alisema wajumbe wameonyesha namna ambavyo hata
mtu wa chini anaweza kushinda tofauti na inavyozungumzwa.
Alisema
wao watu ambao wamekuwa wakizungumza pembeni ukiwa Chama cha Mapinduzi
huwezi kupata nafasi ya uongozi kama hauna fedha jambo ambalo sio kweli
kwa kuwa yeye amechaguliwa bila kujali kipato chake na kuwashinda
walioonekana na kipato cha juu na majina makubwa.
“Niwashukuru
sana wajumbe kwa kunipigia kura za kishindo na kunifanya niibuke
mshindi kati ya wagombea wengine 9 wanachma wenzangu ambao nilikuwa
nikishindana nao ndani ya uchaguzi huu.(P.T)
“2010 nilikuja kwa mara ya kwanza kuwaomba nafasi hii lakini kura hazikutosha lakini safari hii mmeamua kunichagua mimi muuza dagaa na kuudhilihisha umma ndani ya CCM hata mtu wa hali ya chini anaweza kupewa uongozi. Kwa jinsi mlivyoniamini naomba niwahakikishie sitawaangusha na kikubwa naomba tupeane ushirikiano na pale nitakapofanikiwa kuingia bungeni nitakuwa mstari wa mbele kuzungumzia masula yanayowahusu wanawake katika kufanikisha chachu ya maendeleo,”alisema Agnes.
Wakati
akiomba kura kabla ya kuchaguliwa, mgombea huyo aliwatoa chozi wajumbe
baada ya kuomba kura huku akilia akiomba kuchaguliwa muuza dagaa kwa
kuwa kwa kipindi chote amekuwa yupo na wajumbe katika kiangazi na mvua.
Katika
uchaguzi huo, Agnes Methew alichaguliwa kwa kupata kura 418 kati ya kura
641 zilizopigwa na kufuatiwa na Chrstina Samo aliyepata kura 226 huku
Mwenyekiti wa (UWT) mkoa wa Mara, Nancy Msafiri akipata kura 208 na
kushika nafasi ya tatu.
Awali
akizungumza kabla ya kuanza kwa mkutano huo,msimamizi wa uchaguzi,Samwer
Kiboye, aliwahasa wagombea wote kukubalina na matokeo kwa kuwa uchaguzi
ni wa haki ili kuweza kushirikiana kwa pamoja kutafuta kura za CCM
katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba.
via Shommi Binda, blog
0 comments :
Post a Comment