Mbunge Wa Karatu kwa Tiketi ya CHADEMA Ajitoa Rasmi Katika Siasa........Atangaza Kurudi Katika Kazi yake ya UCHUNGAJI

Wednesday, July 22, 2015

Nkupamahmedia

Mbunge wa Karatu kwa tiketi ya Chadema, Mchungaji  Israel Natse, amejitoa rasmi katika siasa na kurudia kazi yake ya uchungaji katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini.

Akizungumza na mtandao huu kwa njia ya simu ya kiganjani jana, alisema makubaliano yake na chama walimwomba agombee kipindi kimoja tu na sasa anapisha mwingine.

“Mimi ninarudi kwenye kazi yangu ya uchungaji naachana na siasa, huu ndiyo wito wangu nilioitiwa na mungu wa uchungaji,” alisema.  
 
Akizungumza kwa njia ya simu ya kiganjani, Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha, Calist Lazaro, alisema kwa Jimbo la Karatu waliochukua fomu za kugombea ubunge ni Lazaro  Masai, Fransisca  Duwe, William Kumbalo, Kwamala  Aloyce na Pascal Gutt.
Nkupamahmedia
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment