Profesa Agnes Mwakaje wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akimvika kofia
ya kitaaluma Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa hafla fupi ya
kumkabidhi Rasmi Rais Joho na cheti cha shahada ya heshima ya Doctor of
Laws(Honoris Causa) ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Makamu wa Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza
Mukandala akimkabidhi Rais Dkt .Jakaya Mrisho Kikwete cheti cha Shahada
ya Heshima ya Doctor of Laws(Honoris Causa) wakati wa hafla fupi ya
kumkabidhi Rais joho na cheti iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam na
kuhudhuriwa na maprofesa waandamizi wa chuo hicho.Tayari Rais Kikwete
alishatunukiwa shahada hiyo katika mahafali ya 41 ya UDSM yaliyofanyika
Octoba mwaka 2011.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandala
akisoma maelezo mafupi baada yeye na jopo la maprofesa waandamizi wa
chuo hicho kumkabidho Joho la taaluma na cheti cha Shahada ya heshima ya
Doctor of Laws(Honoris Causa) ya chu kikuu cha Dar es Salaam wakati wa
hafla iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandakla pamoja
na maprofesa waandamizi wa chuo hicho muda mfupi baada hafla fupi ya
kumkabidhi Rais Joho na Cheti cha Shahada ya Heshima ya Doctor of
Laws(Honoris Causa) ikliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo(picha
na Freddy Maro)


0 comments :
Post a Comment