Umoja wa Afrika umeunga mkono mpango wa kujiondoa kwa pamoja katika
mahakama ya ICC ambayo mataifa mengi ya Afrika yanahisi inawalenga
viongozi wa Bara la Afrika pekee.
Uamuzi huo uliochukuliwa katika kikao cha faragha haujahalalisha hatua hiyo.
Viongozi wa Afrika wanasema kuwa mahakama hiyo ilikosea kumlenga rais wa
Sudan Omar El Bashir kwa mauaji ya Darfur na Uhuru Kenyatta wa Kenya
kwa kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi.
Mpango huo unapendekeza kwamba mataifa ya Afrika yanafaa kuimarisha
mahakama zake na kupanua uwezo wa mahakama ya Afrika kuhusu haki na haki
za binaadamu.
CHANZO: BBC SWAHILI
0 comments :
Post a Comment