Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Burundi
(FFB), Reverien Ndikuriyo anatarajiwa kuwasili leo saa 5 usiku jijini Dar es salaam kwa shirika la Ndege la Rwanda Air.
Ndikuriyo anatarjaiwa kuwa na
mazungumzo na Rais wa TFF, Jamali Malinzi kisha atashuhudia michuano ya
kombe la Kagame inayoendelea kutimua vumbi jijini Dar es salaam ikiwa
katika hatua ya robo fainali kwa sasa.
Aidha Vicent Nzamwita Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Rwanda (FERWAFA) anatarajiwa
kuwasili nchini alhamis akiambatana na kocha wa timu ya Taifa ya Rwanda
(Amavubi) John McKinstry.
Rais wa FERWAFA anatarajiwa kuwa
na mazungumzo na Rais wa TFF, Jamal Malinzi na baadae kuhudhuria
michuano ya Kombe la Kagame inayoendelea nchini Tanzania

0 comments :
Post a Comment