Bingwa wa mita 1500, Basil John kutoka Jeshi la Polisi
Tanzania akimaliza mbio katika uwanja wa Mavuso mjini Mbabane Swaziland
ambapo alifanikiwa kuchukua nafasi ya katika michezo ya majeshi ya
Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika(SARPCCO) inayoendelea nchini
Swaziland.(Picha na Frank Geofray wa Jeshi la Polisi-Swaziland)
Bingwa wa mita 1500, Basil John kutoka Jeshi la Polisi
Tanzania akipongezwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi la Swaziland baada ya
kumvalisha medali ya dhahabu katika michezo ya majeshi ya Polisi kwa
nchi za Kusini mwa Afrika(SARPCCO) inayoendelea nchini Swaziland.(Picha
na Frank Geofray wa Jeshi la Polisi-Swaziland)
………………………………………………………………………………..
Na. Frank Geofray-Jeshi la Polisi,Swaziland.
Mwanariadha
wa Polisi Tanzania, Basil John amefanikiwa kupata medali mbili za
dhahabu baada ya kushika nafasi ya kwanza katika mbio za mita 1500 na
mita 800 katika Michezo ya tisa ya Majeshi ya Polisi kwa nch i za Kusini
mwa Afrika (SARPCCO) inayoendelea katika mji wa Mbabane Swaziland.
Mwanariadha
huyo aliweza kuwashinda wanariadha wenzake baada ya kutumia dakika
1:49:00 katika mbio za mita 800 na katika mbio za mita 1500 aliweza
kutumia dakika 3:49:02 na kuwaacha kwa mbali wanariadha kutoka nchi ya
Zimbabwe na Swaziland ambao walionyesha ushindani mkubwa.
Mwanariadha
mwingine kutoka Tanzania aliyeweza kupata medali ya dhahabu ni Fabian
Nelson katika mbio za mita 5000, ambapo aliweza kutumia dakika 14:27:33
na hivyo kuifanya bendera ya Tanzania kupepea vyema katika michezo hiyo.
Ushindani
mkubwa katika riadha upo kati ya Zimbabwe, Tanzania, Namibia na
Swaziland ambapo nchi ya Swaziland imekuwa ikifanya vizuri katika mbio
fupi.


0 comments :
Post a Comment