Friday, July 17, 2015
Nkupamahmedia
Ray ameiambia Mpekuzi kuwa anasikitishwa na watu wanaodai kuwa
anajichubua bila kujua kuwa mtu akiwa na maisha mazuri anaweza
kubadilika.
“Kwanza sijichubui, tatizo unajua baadhi ya watanzania wengi,
hawaelewi mimi sijichubui, ila maisha yamebadilika,” amesema.
“Unajua
unapokuwa na maisha magumu ya kwanza, unaposhindwa kujikimu,
kujinunulia nguo, yaani kufanya unachokitaka kwa muda unaoutaka, unakuwa
mweusi kwa sababu huna hela ya kujikimu, sasa unapopata pesa kidogo ya
kujikimu, unapokuwa na maisha mazuri , kwako kuna AC, kwenye gari yako
kuna AC, hupati jua huwezi kuwa mweusi,” amesisitiza.
“Pia ukishakuwa star lazima muonekano wako uwe tofauti kidogo ili
uwe tofauti kidogo. Hawa wanaoona mimi najichubua labla wanaona vibaya!
Mimi sijichubui na waache waendelee kuzungumza kwa sababu mtanzania
huwezi kumzuia kuzungumza.”
Nkupamahmedia



0 comments :
Post a Comment