TANZANIA YAELEZEA MATUMAINI YAKE KWA MKUTANO WA UFADHILI WA MAENDELEO


Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Saada  Mkuya Salum akizungumza  katika siku ya pili ya mkutano wa tatu wa kimataifa kuhusu ufadhili wa  maendeleo ( FFD3) unaoendelea jijini Addis Ababa- Ethiopia
Na   Mwandishi Maalum, 
New York
Mkutano wa tatu wa kimataifa  kuhusu ufadhili wa maendeleo, ( FFD3) jana (jumanne) umeingia siku yake   pili ambapo  Waziri wa  Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Saada   Mkuya Salum alielezea matumaini ya   Tanzania  juu ya matokeo ya mkutano huo katika kusukuma mbele ajenda ya maendeleo endelevu.
 Waziri   wa Fedha ambaye anamwakilishi  Mhe. Rais Jayaka Mrisho Kikwete katika mkutano huo,  amesema kuwa,  Tanzania  inaamini  kwamba ufadhili wa  maendeleo ni moja ya ajenda muhimu kwa Bara la Afrika .  Kwa sababu hiyo Tanzania,   inategemea  kuona ufadhili huo  unakuwa na  matokeo makubwa   katika kuondoa umaskini katika   nchi nyingi za Afrika.
“  Kama kweli  tunataka kuwa na utekelezaji wa uhakika wa  malengo ya maendeleo endelevu baada ya 2015, Matumaini ya  nchi yangu ni kuona   kuwa mkutano huu unatoka na  matarajio mathubuti yatakayo hakikisha mtiririko  usio shaka wa  rasilimali kuchagiza maendeleo”. Amesema Mhe.Waziri
          Ametoa  wito wakuwapo kwa    mikakati ya   pamoja  baina ya   pande zote, kule zitokako au  asili ya  raslimali  hizo na  nchi zinazopokea misaada hiyo  lengo  likiwa  kudhibiti  mrititiko wa fedha chafu, uwezeshwaji wa kukomboa raslimali na kuzirejesha  raslimali  hizo kwa nchi husika.
“ Afrika inapoteza  karibu  dola  bilioni 50 kwa mwaka kutokana na  mtiririko wa fedha chafu kutoka nchi zinazoendelea,  hali inayosababisha  kusababisha uhaba mkubwa wa   hazina ya fedha za kigeni,  kupungua kwa makusanyo ya kodi,  kufutwa  vyanzo vya uwekezaji uwekezaji na hatimaye kuongezeka kwa umaskini”. Amesema  Waziri  wa Fedha.
Kiongozi huyo wa ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo,  ameelezea umuhimu wa    Mkakati wa Addis Ababa kujielekeza  na kuwa mfumo  madhubuti utakaoimarisha ushirikiano katika masuala  ya kodi.
 Vile vile Waziri wa fedha,  amesisitiza kwamba takwimu zitakazotumiwa na Taasisi ambazo zitapewa  jukumu la  kufuatilia na kufanya marejeo  kuhusu ufadhili  wa maendeleo , takwimu hizo ni  lazime zitoke  katika   taasisi za takwimu ambazo zinatambuliwa na serikali ya nchi husika.
Akabinisha kwamba  matumizi ya  takwimu  rasmi kutoka  taasisi zinazotambuliwa na serikali , kutaepusha  kutumiwa  kwa takwimu  ambazo si rasmi na hivyo kusababisha sitofahamu  na migongano  kati ya  Nchi wanachama na   Umoja wa Mataifa.
Waziri Saada Mkuya Salumu  akatoa wito   wa   kuongezwa raslimali fedha  hususani kwa nchi  zinazoendelea   ili ziwe  na uwezo wa kuboresha mifumo  yake ya  ukusanyaji wa takwimu, kuzichambua na kuzifanyia tathmini.

MONUSCO YAHITAJI USHIRIKIANO WA KARIBU ZAIDI NA DRC

  Na Mwandishi Maalum, New   York
Uwezo wa  Misheni ya   Ulinzi wa Amani katika   Jamhuri ya  Kidemokrasia ya Kongo ( MONUSCO) wa kutekeleza  mamlaka yake kikamilifu  utategemea zaidi  ushirikiano na uhusiwano wake na mamlaka za  nchi hiyo.
Hayo yameelezwa na  Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  katika DRC,  Bw. Martin Kobler wakati alipowasilisha  taarifa yake  mbele ya   wajumbe wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa  Mataifa  siku ya jumaane.
 Taarifa    Bw. Kobler kwa  Baraza hilo ilihusu maeneo matatu ambayo ni  uchaguzi mkuu utaotarajiwa kufanyika  mwakani,  hali ya  usalama  na mkakati wa  upunguzaji wa idadi ya walinzi wa Amani.
“ Mafanikio ya  utekelezaji wa mamlaka yetu unategemea na kuendelea kwa  majadiliano na ushirikiano  na serikali  na hususanu  kuhusu hali  ya usalama katika eneo  la  Mashariki na  Mchakato wa Uchaguzi.
Akielezea zaidi  kuhusu hali ya  usalama,  Mwakilishi  wa Katibu Mkuu,  ameliambia  Baraza kwamba,  kuna matumaini katika baadhi ya  maeneo. Akibainisha  juu ya operesheni zinazoendelea   dhidi ya kundi la wanamgambo  la   Force  de Resistance Patriotique en Ituri ( FPRI) na zinazofanywa  na   Jeshi la  DRC  ( FARDC) kwa kusaidiwa na  MONUSCO.
“ Wakati kipaumbele ni kuhakikisha kuwa kundi  hili linasalimisha  silaha kwa hiari, matumizi ya  nguvu ilibidi yafanyike baada ya kunvujwa  mara tatu muda wa mwisho ambao kundi hilo  lilipashwa kusalimisha  silaha zake kwa hiari” amesema Bw. Kobler
Kuhusu operesheni ya pamoja dhidi ya kundi la  Force Democratique de Liberation du Rwanda ( FDLR) katika  maeneo ya Kivu  Magharibu,  Kivu ya Kusini na  Katanda  amsema operesheni hiyo  imesimama kwa zaidi ya miezi mitano.
 Amefafanua kuwa  kusimama kwa  operesheni  hiyo ambayo ilitakiwa ifanywe na  FARDC kwa kusaidiwa na MONUSCO   licha ya kwamba  pamoja na mambo mengine kulitoka na   hoja ya  awali kuhusu  haki za binadamu bali sasa limekwenda mbali zaidi ya hapo.
Akaongeza kwamba wakati  MONUSCO ikirejea na kufanya tathmini kuhusu haki za binadamu ilikuwa inatafuta njia ya namna ya kuendeleza ushirikiano kupitia mpango uliopo sasa.
Akielezea zaidi kuhusu hali ya usalama,  Bw. Martin Kobler amesisitiza kuwa wakati  serikali  ya DRC imepiga hatua kubwa katika  kurejesha hali ya Amani  katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo. Bado wananchi wa  eneo la  Mashariki ya  nchi hiyo maisha yao yanategemea sana huruma ya makundi ya wanamgambo wenye  silaha.
 Pamoja na  mafanikio  ya  kupunguza  nguvu ya  FDLR katika baadhi ya  maeneo waliyokuwa wakiyakalia, jeshi la DRC limejikuta  katika mazingira magumu ya  kuyadhibiti  na kuyashikilia maeneo yaliyokombolewa na kwamba hakuna muda wa kusubiri.
Kuhusu  uchanguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika  mwezi Novemba  mwaka 2016, Bw. Kobler amesema wajibu wa kuhakikisha kwamba uchaguzi huo unakuwa wa huru, haki na wazi ni wa serikali yenyewe ya DRC
Akaongeza kwamba  tajio  la haraka   katika kuhakikisha kwamba uchaguzi  utafanyika kwa  wakati ni fedha , kalenda sahihi ya  uchaguzi,  uboreshaji wa daftari la wapiga kura na utoaji wa  fursa kwa vyama vya upinzani. Akamsifu  Rais Kabila kwa kupanua wigo wa majadiliano na  wadau mbalimbali  katika kipindi  cha kuelekea uchaguzi.
Katika hatua nyingine.  Mwakilishi wa Jordan na ambaye ni  Mwenyekiti wa Kamati ya  Vikwanzo dhidi ya DRC, Dina Kawar , ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania kwa kumkamata  na kisha kukubali  kumpeleka   nchini Uganda   kiongozi wa Kundi la  Allied Democratic Force ( ADF) Bw. Jamil Mukulu

Ametoa shukrani hizo wakati naye alipokuwa akiwasilisha taarifa ya  Kamati yake mbele ya  Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment