SHINDANO la kusaka vipaji lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT) 2015 wiki hii limezidi kufikia patamu baada ya washiriki 15 kubaki kati ya 20 waliokuwa wameingia katika Jumba wakati wiki hii ikishuhudia surprise ya washiriki kupigiana kura wao kwa wao.
Washiki hao wa TMT kila wiki wanapata mafunzo ya sanaa kwa nadharia na vitendo kutoka kwa waalimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambao ni Dkt. Mona Mwakalinga na Issa Mbuya kisha hupewa ‘script’ ya kuigizia.
Majaji na walimu hupitia mapema ‘script’ hizo ili kuangalia ushiriki wa kila mmoja na kuona uwezo wake tofauti na siku zilizopita, kitu kinachoamua uwepo wa kila mshiriki.
Vilevile baada ya hapo mchujo kwa washiriki wawili hufanyika kwa ajili ya kuyaaga mashindano kwa aliye na kura chache na kuigiza chini ya kiwango.
Ili mshiriki unayempenda aendelee kubakia ndani ya Jumba la TMT 2015 na kumpa nafasi ya kushinda milioni 50, katika simu yako ya kiganjani, andika TMT, acha nafasi, namba ya mshiriki kisha tuma kwenda 0784367738.?
Majina na namba za washiriki katika mabano ni Nadhifa Haruna (01), Aisha Katabazi (02), Kalombo Amboni (04), Dennis Laswai (05),
Tomluck Stephan Shukuru (06), Catherine Nicholaus (07), Titus Maridhia (08), Daniel Lufingo (09), Vandeline August (11), Jackson Sakumi (12), Naomi Chuwa (13), Sadam Nawanda (14),
Mohamed Massanga (15), Saidi Bakari Mbelemba (16) na Rachel Michael (17).
(Hababri: Denis Mtima/Gpl)


0 comments :
Post a Comment