- Written by Nkupamah blog
-

MWIMBAJI
nguli wa muziki wa Injili Tanzania, Upendo Nkone amekuwa wa kwanza
kujitokeza kusindikiza uzinduzi wa mwenzake Bonny Mwaitege,
utakaofanyika Agosti 2 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es
Salaam.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama Nkone
amekuwa wa kwanza na ameonesha nia ya kumsindikiza Mwaitege kwa sababu
ya ubora wa uzinduzi huo. “Uzinduzi wa Mwaitege utakuwa ni wa aina yake
kwa sababu maandalizi yake kwa yamefanywa kwa ustadi mkubwa hasa hatua
za mwisho za rekodi ya albamu hizo inayomaliziwa jijini Mwanza na
baadaye Nairobi,” alisema Msama.
Msama
alisema Mwaitege anatarajia kuzindua albamu tatu ambazo zitashika anga
la muziki huo hapa nchini kwa sababu ya ubora. Msama alisema sambamba na
muimbaji huyo, mikoa mbalimbali imeonesha nia ya kutaka uzinduzi wa
albamu hizo.
Aidha
Msama alitoa wito kwa mashabiki wa muziki wa Injili Tanzania kujiandaa
kupata neno la Mungu kupitia muimbaji huyo. Bonny Mwaitege anatamba na
nyimbo mbalimbali kama Mama ni Mama, Mke mwema, Wakusamehe, fungua moyo
wako na njoo uombewe na Yesu yupo.(VICTOR)


0 comments :
Post a Comment