Mwimbaji nguli wa muziki wa
injili Bonny Mwaitege akiimba katika uzinduzi wa albam zake kwenye
ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam jana, uzinduzi ambao
ulihudhuriwa na maelefu ya wapenzi wa muziki wa ijini akishirikiana na
waimbaji mbalimbali wa muziki huo ikiwa ni pamoja na baadhi ya kwaya
kutoka katika baadhi ya makanisa ya jijini Dar es salaam, Bonny Mwaiteje
alikonga nyoyo za mashabiki wake kwa ikwango kikubwa huku akiwa
amevalia vazi la Kingigeria wakati akiwa jukwaani, wapenzi wa ,muziki
waliohudhuria katika uzinduzi huo walijikuta kila mmoja akijitikisa pale
alipo kutokana na kuvutiwa na nyimbo za mwimbaji huyo kutoka mkoani
mbeya.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Mwimbaji nguli wa muziki wa
injili Bonny Mwaitege akitunzwa na wapenzi mbalimbali wa muziki wa
injili wakati alipokuwaa akiimba jukwaani.
Baadhi ya maaskofu na wachungaji waliohudhuria katika uzinduzi huo wakifuatilia wakati mwimbaji huyo akiimba jukwaani.
Mwimbaji nguli wa muziki wa injili Bonny Mwaitege akifanya mabo makubwa jukwaani.
Baadhi ya wapenzi wa muziki wa injili wakiwa katika uzinduzi huo.
Askofu na Dokta Mwakibolwa wa
EAGT pamoja na maaskofu wenzake wakiombea albam hizo kabla ya
kuzizindua rasmi kushoto ni Alex Msama Mkurugenzi wa Kamuni ya Msama
Promotion.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Msama Promotion wakishiriki katika sala.
Sala ikiendelea kabla ya kuzinduz albam hizo.
Baadhi ya wapenzi wa muziki wa injili wakiwa katika uzinduzi huo uliofanyika jana kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.
Askofu na Dokta Mwakibolwa wa EAGT akizindua rasmi albam hizo kushoto Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama.
Maaskofu na wachungaji wakiwa wameshikilia albam zao mara baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion.
Baadhi ya wafanyakazi wa Msama Promotion wakiwa katika picha ya pamoja.
0 comments :
Post a Comment