NDEGE ZA FASTJET ZAKATISHA SAFARI ZAKE KUFUATIA TATIZO LA UMEME KATIKA UWANJA WA NDEGE WA MWANZA

indexKufuatia tatizo la kiufundi la umeme katika uwanja wa Ndege wa Mwanza ambalo lilisababisha ndege za kampuni ya Fastjet kukatisha safari zake zote za usiku kuepuka kuhatarisha maisha ya abiria na wafanyakazi, tunapenda kuwashukuru wateja wetu wote kwa ushirikiano wao na uvumilivu waliotuonyesha na tunawaomba wawasiliane nasi ili kupata maelezo zaidi juu ya safari zao.
Wakati mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania ikiendelea kufanya juhudi za kutatua tatizo hili,  safari zetu za usiku za kuingia na kutoka jijini Mwanza zinaendelea kusitishwa na tutawapa maelezo zaidi mapema iwezekavyo huduma zetu zitakaporejea.
Tunawataarifu kuwa safari zetu za mchana zinaendelea kikamilifu na wateja wa Fastjet wana haki ya kuahirisha safari zao zilizositishwa au kupata tiketi nyingine ndani ya siku saba kuanzia leo au kudai pesa kwa tiketi zozote ambazo hazikutumika.
Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza na tunapenda kuwahakikishia wateja wetu kwamba, usalama wao ndio wajibu wetu mkubwa!
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment