Deo Filikunjombe (CCM)
fomu ya mgombea wa Chadema ubunge Ludewa zikiwa hazijatimia baada ya fomu ya tamko kukosekana
Mzee Kada wa Chadema akimpongeza mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe baada ya kupewa barua ya kupita bila kupingwa
Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe akizungumza na wanachama
wa CCM na wananchi wa Ludewa baada ya kupita bila kupingwa
Filikunjombe akionyesha barua ya kupita bila kupingwa .
Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Ludewa Bw Wiliam Waziri akimpongeza mbunge Filikunjombe baada ya kumkabidhi barua ya kupita bila kuingwa ubunge jana. |
Na matukiodaimaBlog Ludewa
ALIYEKUWA mbunge wa jimbo
la Ludewa Deo Filikunjombe (CCM) amepita bila kupingwa baada
ya mgombea wa chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema) Barthomew
Mkinga kushindwa kutimiza Masharti na Taratibu za Ujazaji wa Fomu.
Msimamizi
wa Uchaguzi Wilaya ya Ludewa Bw Wiliam Waziri alisema jana kuwa
Mgombea wa Chadema ameshindwa kutimiza taratibu za ujazaji wa fomu hizo
hivyo kukosa sifa ya kuwa Mgombea wa Ubunge
hivyo kumkabidhi barua rasmi Filikunjombe ya kupita bila kupingwa
Waziri alisema kwamba Kati ya wagombea wanne waliochukua fomu aliyetimiza taratibu ni Mgombea wa CCM, Bw. Filikunjombe pekee;
Kuwa
Wagombea wa DP na TLP walishindwa kabisa kurejesha fomu huku Mgombea wa
Chadema akishindwa kujaza fomu vizuri na kushindwa kurejesha Fomu ya
Kiapo cha Maadili ya Sheria za Uchaguzi.
Mgombea huyo wa
Chadema aliyereja fomu ya wadhamini bila kujaza
tarehe ,mwezi wala mwaka ambao uchaguzi mkuu utafanyika .
Kwa upande wake mgombea ubunge wa
TLP Bw Blanka Haule alisema kuwa alishindwa kurejesha fomu
hizo kwa wakati kutokana kukosa picha za kubandika katika fomu
hiyo kutokana na hali ya mazingira ya Ludewa kukowa eneo
la kupiga picha hizo.
Kwani alisema
picha ambazo
alipiga Njombe alizisahau alikoziweka hivyo kulazimika kwenda kupiga pich
nyingine za haraka kwa muda wa dakika tatu ila cha kushangaza
dakika tatu za kutoka picha hizo zilionekana kushindwa kutoka
kwa wakati na kutoka saa 11 jioni .
“Nilijipanga kugombea ubunge ili kumpokea ubunge Deo
Filikunjombe na kuendeleza yale yote aliyoyafanya jimboni ila
watu wa picha walinikwamisha na kushindwa kupata picha kwa wakati
hivyo kwa sasa ndio basi tena japo ilikuwa ni Demokrasia lakini
kapita bila kupingwa ndio mbunge wetu:”
Akizungumzia hatua
ya mgombea wao wa
Chadema kushindwa kukamilisha taratibu za ujazaji wa fomu hizo Bw
Daniel Songo alisema kuwa mgombea wao hakuwa makini hata kidogo kwani
alikuwa ni mtu ambae hakutulia na muda mwingi alikuwa akifikiria juu
ya wanachama wanaohama chama na kuacha kutulia katika
kujaza fomu hizo .
Japo alisema
chama hicho kimepoteza umaarufu kutokana na mwenendo wa viongozi
wa juu wa chama hicho kuendekeza siasa za ukanda zaidi na
kuacha kutazama uhai wa chama hicho.
Mwenyekiti wa
CCM wilaya ya Ludewa Stanle Kolimba alisema kuwa amepokea
kwa furaha kubwa hatua ya mgombea wake wa nafasi
ya ubunge kupita bila kupingwa na kuwa kazi kubwa
kwa sasa kuhakikisha mgombea urais wa CCM Dr John Magufuli
anapata kura za kimbunga pamoja na kupigania kata zote kuona CCM .
Kwa
upande wake Bw Filikunjombe akizungumzia hatua hiyo
ya kupita bila kupingwa alisema ameipokea kwa vizuri sana
kwa alitegemea wapinzani hao wajitokeze ili aweze kuwaonyesha
kazi kwa kuhakikisha wanaangukia pua katika uchaguzi huo .
Alisema
kazi kubwa ya maendeleo ambayo ameifanya katika jimbo hilo kwa
miaka mitano na imani kubwa ambayo wananchi wa Ludewa wanayo dhidi yake
ilikuwa ni vigumu kwa wapinzania hao kupata kura Ludewa.
Bw Filikunjombe aliwaomba wananchi
wa Ludewa
kura zote ambazo walipanga kumpigia yeye kuzielekeza kwa
mgombea Urais Dr Magufuli na kwa madiwani wa CCM na furaha yake kuona
wapinzani wanaambulia patupu katika wilaya ya Ludewa .
Hadi sasa
zipo taarifa kuwa jumla ya majimbo 5 wagombea ubunge wa CCM
wamepita bila kupingwa likiwemo jimbo la Pelamio,Ludewa, Mlalo,
Bumbuli, na Sengerema.
0 comments :
Post a Comment