Kamanda wa Kanda Maalum ya Kipolisi ya Dar es Salaam Kamishna Simon Siro amesema kuwa siku ya kesho Agosti 27, Jeshi hilo la Polisi litatoa taarifa kamili kuhusiana na taarifa zinazozagaa kuhusiana na Majambazi maeneo ya vikindu jiji Dar es Salaam.
Taarifa hizo zinazosambaa kupitia mitandao ya kijamii zinaeleza kuwa kuna uwepo wa majambazi eneo la Vikindu jijini Dar es Salaam ambao wanasilaha nzito za kivita, lakini pia taarifa hizo zinasema kumekuwa na majibizano ya risasi baina ya Jeshi la Polisi na majambazi hao na kuna baadhi yao wamejeruhiwa ama kuuwawa na hata zingine zikieleza kuwa Askari ameuwawa katika majibizano hayo.
Mtandao huu ulipowasiliana na Kamanda Siro, ambapo hata hivyo msaidizi wake amebainisha kuwa watalitolea ufafanuzi suala hilo hiyo siku ya kesho Agosti 27.2016 watakapokutana na Wanahabari majira ya saa tano asubuhi.
Mtandao huu utaendelea kukujulisha kila kitu kadri tutakavyopata taarifa sahihi..
Na Hashim Ibrahim (UDSM-SJMC).
0 comments :
Post a Comment