Jose
Mourinho amesema kwamba atasherehekea kufikisha michezo 100 ya nyumbani
akiwa kama kocha wa Chelsea endapo tu Chelsea atapoteza mchezo wake wa
leo dhidi ya Crystal Palace.
Kocha huyo ana rekodi nzuri sana ya michezo ya nyumbani huku akiwa amepoteza mchezo mmoja tu dhidi ya Sunderland msimu uliopita.
Amesema kuwa atakuwa hana furaha kubwa ya kujigamba mtaani endapo timu yake itaifunga Palace.
“Kama
utaniuliza kuhusu wapi nitapata chakula cha usiku, basi nitakuwa kinyume
kabisa. kama nitapoteza basi nitatoka. Zaidi ya hapo endapo nitashinda,
sitaenda popote. Nina takribani migahawa minne au mitano hivi ambayo
huwa napendelea kwenda”, aliwaambia waandishi.
"Ni kama
kitu cha kifamilia. Sipaswi kujificha kwa sababu nimepoteza mchezo,
hivyo ni kuifanya familia yangu iwe na huzuni zaidi kutokana na matokeo
hayo kwa sababu nimepoteza, na kukaa tu nyumbani eti kwa sababu
tumefungwa, hapana siwezi kufanya hivyo.(VICTOR)
0 comments :
Post a Comment