Ndugu zangu,
Kwenye
Nchi ya Kusadikika, miongoni mwa hulka mbaya zinazowatesa Wasadikika ni
pamoja na kuendekeza sana fitina na unafiki. Wasadikika hawaaminiani.
Wasadikika
hawapendi pia kuambiwa ukweli. Kwenye shida yake, Msadikika akikufuata
kukuomba msaada au ushauri, basi, anachotaka kusikia kutoka kwako ni
maneno matamu ya kumjaza matumaini, na hata kumsifia kwa kisichokuwepo
kiuhalisia. Ukimwambia ukweli atakasirika.
Anaweza hata kupita mitaani na kukusema; " Yule bwana bure kabisa, afadhali hata angeniongopea tu!"
Na ajabu
ya Wasadikika ni kuwa, zamani sana walikubaliana na kulishana yamini,
kwa mdomo na kwa maandishi, kuwa kwenye Nchi ya Kusadikika watakuwa "
Wakisema Kweli Daima, Fitina Kwao Mwiko".
Leo hii,
sio tu Wasadikika wameshasahau makubaliano yao hayo, bali, wana hata
viongozi wao ambao hawajui kama kulipata kuwepo kwa makubaliano hayo!
Naam,
Wasadikika wako katikati ya mkanganyiko mkubwa kupata kutokea tangu
kuanzishwa kwa taifa lao. Na kuna Wasadikika wenye kuamini, kuwa Mungu
anawapenda zaidi Wasadikika, na kwamba atawaletea ' Nabii' wa
kuwakomboa...!
MaggidShauri Moyo,
Mji Kwenye Nchi Ya Kusadikika.(P.T
0 comments :
Post a Comment