Saturday, August 1, 2015
@nkupamah blog
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi namba 301 iliyofunguliwa na Kampuni ya kufua Umeme ya IPTL, PAP pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya PAP Bw Harbinder Singh Sethi dhidi ya Mbunge wa Kigoma Kusini, Mhe David Kafulila.
Kesi
hiyo illikuwa ikidai kuwa Kafulila alichafua jina la kampuni hizo na
mhusika wake kwamba walichota zaidi ya shilingi bilioni 300 kwenye
akaunti ya Tegeta escrow kinyume cha sheria na taratibu.
Katika
shauri hilo, Kampuni ya IPTL, PAP na Herbinder Singh Sethi walitaka
Mahakama imwamuru Kafulila ailipe fidia ya sh. 310bn kwa kuchafua jina
la kampuni na mkurugenzi huyo.
Katika
kesi hiyo Kafulila alikuwa akitetewa na taasisi za kisheria za Legal
& Human Rights Centre pamoja na kituo cha Human Rights Defenders.
Akitoa
uamuzi huo mbele ya mawakili wa Human Rights Defenders na Legal &
Human Rights Center wakiongozwa na wakili Mtobesya huku mawakili wa
IPTL, PAP na Sethi wakiwa hawakufika mahakamani, Jaji Rosemary Teemba
alisema Mahakama Kuu imejiridhisha kwamba kampuni ya IPTL, PAP na
Mkurugenzi wao Harbinder Sethi hawakuwa na hoja za msingi kuthibitisha
madai yao kama msingi wa kufungua kesi mahakama kuu na hivyo kwa
kuzingatia hayo, Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam inatupilia mbali
shauri hilo.
@nkupamah blog
0 comments :
Post a Comment