Sunday, August 2, 2015
@nkupamah blog
Wakati Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Party (DP), Christopher Mtikila akigoma kusaini fomu za kugombea urais akitaka ufafanuzi wa mgombea binafsi, Mwenyekiti wa UPDP, Fahmi Dovutwa amekwama kwenye lifti za jengo lililopo katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi (NEC) kutokana na kukatika umeme.
Mchungaji
Mtikila ambaye aliambatana na mgombea mwenza Juma Metu Juma, alitaka
ufafanuzi wa kutokuruhusiwa kuwania urais akiwa mgombea binafsi wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati Mahakama ya Haki za Binadamu ya
Afrika (AfCHPR) imeruhusu.
“Siondoki
hapa na wala sitaweza kuchukua hizi fomu hadi mniambie ni wapi nitapata
jibu la tume la kukiuka maagizo ya mahakama ya Afrika.
“Waandishi
embu subirini kwanza mkurugenzi wa uchaguzi aje hapa ili atoe ufafanuzi
na nyie msikilize mkaandike ukweli kwa sababu hii siyo haki ni sawa na
kudharau mahakama,” alisema.
Baada
ya kuzozana na maofisa waliokuwa wakimkabidhi fomu hizo, walilazimika
kumuita mkurugenzi wa uchaguzi Kailima Ramadhani, ambaye alimwambia
kwamba sheria hairuhusu.
“Sisi
tunafuata sheria mwenyekiti kama hicho kipengele kingekuwapo
tungekuruhusu uchukue fomu hizo, lakini hapa tunabanwa na sheria
tunaruhusu kutoa fomu kwa watu wanaotoka kwenye vyama vyao,” alisema Ramadhani
Alisema
ni vizuri Mtikila angefuatilia kwa makini suala hilo ili sheria
ipitishwe kwani NEC wanachokifanya ni kufuata sheria zilizopo tu na si
vinginevyo.
Baada
ya kumaliza maongezi Mtikila aliamua kuweka sahihi na kuchukua fomu
hizo kwa shingo upande huku akisema atakiwakilisha vyema chama chake
hicho.
Juni
13,2013 Mtikila alishinda kesi aliyofungua AfCHPR, mjini Arusha akidai
Tanzania inakiuka demokrasia inapozuia wagombea binafsi.
Mchungaji
Mtikila, ambaye ana historia ndefu ya kukwaruzana na Serikali ya Chama
cha Mapinduzi (CCM), alifungua shauri mahakama ya Afrika mwaka 2011
baada ya jitihada zake za kupindua mabadiliko ya kikatiba yaliyofuta
ugombea binafsi kugonga mwamba kwenye mahakama za kitaifa.
Dovutwa
Mwenyekiti wa UPDP Fahmi Dovutwa alikwama kwenye lifti kwa dakika kumi baada ya jana kuchukua fomu za kuwania urais.
Dovutwa
ambaye alikuwa wa kwanza kufika kuchukua fomu saa tatu asubuhi, akiwa
ameambatana na mgombea mwenza, alisema kwamba kukwama kwake kwenye lifti
ni hujuma iliyofanywa na baadhi ya wagombea wenzake wa urais.
Wakati
huohuo; Mgombea urais kwa tiketi ya TLP Maxmilian Lyimo, ambaye hakuwa
na mgombea mwenza alikuwa wa pili kufika katika ofisi hizo kwa ajili ya
kuchukua fomu.
Mgombea
huyo alifika saa 5:33 asubuhi baada ya kuchukua fomu alisema kuwa upepo
wa Uchaguzi Mkuu unaovuma mwaka huu, haukuwahi kuvuma wakati mwingine
wowote, hivyo inaashiria kuwa nchi itapata kiongozi asiyetarajiwa na
wengi.
“TLP
ni chama kisichochafua amani tangu kuasisiwa kwake, hivyo wananchi
waangalie amani ya nchi kwani ni bora kuliko kitu kingine,”alisema na kuongeza:
“TLP
bado kuna nafasi za uongozi kuanzia kata hadi za ubunge, wanaoshindwa
huko waliko tunawakaribisha kwa ajili ya kuja kugombea nafasi hizo.”
@nkupamah blog



0 comments :
Post a Comment