Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la
Chama cha Skauti Tanzania unatarajiwa kufanyika jijini D’salaam kuanzia
tarehe 13 Agosti hadi 15 Agosti 2015 katika ukumbi wa Karimjee. Mkutano
wa Baraza Kuu hufanyika kila baada ya miaka 2 na mara ya mwisho
ulifanyika mwaka 2013 jijini D’salaam. Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu
utatanguliwa na Semina Elekezi kwa wajumbe wote wa Baraza Kuu, ambao
itaanza tarehe 13 na 14 Agosti 2015 na Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu Taifa
utafanyika tarehe 15 Agosti 2015.
Wajumbe wote wa Baraza wanatakiwa
kuripoti jijini D’salaam tarehe 12 Agosti 2015 jioni. Wajumbe wa Baraza
Kuu ni pamoja na Makamishna wote wa Skauti wa Mikoa na Wilaya za
Tanzania, Wakufunzi, Viongozi wa Juu wa Chama, pamoja na wageni wengine
waalikwa. Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu unatarajia ufunguliwe na Mlezi wa
Chama cha Skauti Tanzania ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.
Viongozi wengine wa juu wa Chama
ni pamoja na Wadhamini ambao ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mheshimiwa
Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu Salim Ahmed Salim na Baba Askofu
Timanywa. Rais wa Baraza la Chama cha Skauti Tanzania ni Waziri wa
Elimu Mheshimiwa Dk. Shukuru Kawambwa na Makamu wake ni Kaimu Mufti wa
Tanzania Alhaji Zuberi, Muadhama Kadinali Polycap Pengo na Profesa
Philemoni Sarungi.
Viongozi wengine wa Juu wa Chama
ni pamoja na Skauti Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mwantumu Mahiza, ambaye
pia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Kamishna Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania
Mheshimiwa Abdulkarim Shah ambaye pia ni Mlezi: RAIS WA JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA Patron: THE PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF
TANZANIA P.O. BOX. 945 DAR ES SALAAM, TEL: +255222153342 FAX: + 255 222
150382 EMAIL: tscouts2002@gmail.com TANZANIA SCOUTS ASSOCIATION CHAMA
CHA SKAUTI TANZANIA Mbunge wa Mafia na Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji
ya Taifa Mheshimiwa Balozi Mstaafu Nicholas Kuhanga. Mkutano Mkuu wa
Baraza Kuu pamoja na mambo mengine utajadili na kupitisha Katiba ya
Chama cha Skauti Tanzania, pamoja na kuchagua wajumbe wa Kamati ya
Utendaji ya Taifa.
Fomu za wagombea nafasi hizo
tayari zinapatikana Makao Makuu ya Skauti Tanzania yaliyopo upanga,
barabara ya Malik, pia katika blog na Tovuti ya Chama ambayo ni
www.tanzaniascout.org Mwisho wa kurudisha fomu hizo ni tarehe 7 agosti
2015 saa 9.00 alasiri.
Imetolewa na RASHID K. MCHATTA KNY: KAMISHNA MKUU CHAMA CHA SKAUTI TANZANIA 31/07/2015


0 comments :
Post a Comment