MUFT MKUU WA ZANZIBAR ASISITIZA MASHEKH NA WALIMU KUHUBIRI AMANI


Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi wakwanza kushoto akitoa maelezo juuya haki za binaadamu  kwa mujibu wa Uislam wakati alipokuwa akifunguwa Mafunzo ya Haki za Binaadamu na kuwatambulisha wasaidizi wa Sheria kwa Viongozi wa Dini, katikati ni Mkurugenzi Mtendaji Harusi Miraji na mwisho Jina Mwinyi Waziri Afisa Mipango wa Kituo cha Huduma na Sheria.
Sheikh Thabit Nooman Jongo kutoka Afisi ya Mufti Zanzibar akiwafahamisha jambo washiriki wa mafunzo ya Haki za Binaadamu katika Ukumbi wa Mazsons Hotel mjini Zanzibar

Na Miza Othman –Maelezo Zanzibar         26/08/2015.
Mashekhe na Walimu wa Madrasa wametakiwa kuwashajihisha Wananchi ili waepuke kujiingiza katika makundi yanayoweza kuvunja amani katika kipindi hiki cha Mchakato wa Uchaguzi Mkuu nchini.
Hayo yameelezwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi alipokuwa akifunguwa mafunzo ya Haki za Binaadamu yaliyoandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar na kufanyika katika ukumbi wa Mazsons Hotel,Shangani Mjini Zanzibar.
Amesema Masheikh na Walimu hao ndio Wasimamizi wakuu katika maeneo mbalimbali ikiwemo Miskitini, Madrasani na hata ndani ya Nyumba zao kwani kufanya hivyo kutawasaidia kuepuka Uvunjifu wa Amani ni.
“Tofauti za dini, jinsia, cheo na Kabila sio njia za ukiukwaji wa Sheria ndani ya Nchi yetu bali zitumike katika kutii sharia kwa kila raia”,alisema Shekh Kaabi.
Nae Shekh Thabit Nooman Jongo kutoka Afisi ya Mufti Zanzibar amewataka Walimu na Mashekhe wenzake kuwa mstari wa mbele katika kusimamia juu ya ukumbusho huo kwani kufanya hivyo ni kutekelaza majukumu yao.
Aidha amewataka Masheikhe na Walimu  hao kuchukuwa juhudi za hali ya juu na kutumia maneno ya hekima, busara na unyenyekevu ili waweze kufanikiwa malengo waliyokusudia.
Hata hivyo amesema kuwa wakati wanapotoa hutuba zao ndani ya Misikiti na Madrasa ziwe ni zenye kujenga amani kwani kufanya hivyo ni kuzitii sheria zilizowekwa katika nchi yao.
Kwa upande wao Washiriki wa mafunzo hayo wamesema watayafanyia kazi bila ya kinyongo na kuyafikisha katika maeneo yao kama walivyoagizwa na Viongozi wenzao.
                IMETOLEW NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment