Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,
Dkt. Florens Turuka (mwenye miwani) akimsikiliza Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, Patrick Karangwa wakati alipokagua
ujenzi wa nyumba za waathirika wa maafa Kijijini Mwakata, Kahama,
tarehe 30 Agosti, 2015.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,
Dkt. Florens Turuka akimsikiliza mwenyekiti Kijiji cha
Mwakata wilayani
Kahama, Ezekieli Ramadhani akitafsiri kwa Kiswahili shukrani zizokuwa
zikitolewa kwa kisukuma na Bi. Rugumba Msenga kwa serikali kumjengea
nyumba kutokana na nyumba yake ya awali kuathirika na maafa ya Mvua,
wakati Katibu Mkuu huyo alipokagua ujenzi wa nyumba za waathirika hao
zilizojengwa na SUMA JKT, tarehe 30 Agosti, 2015.
Muonekano wa nyumba mpya ya
muathirika wa maafa ya mvua kijijini Mwakata Kahama. Rugumba Msega
(hayupo pichani ) ambayo amejengewa na serikali kupitia Idara ya Uratibu
Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa usimamizi wa SUMA JKT, kulia ni makazi
ya muda aliyokuwa amejengewa na serikali na mbele ya nyumba hiyo ni
mabaki ya nyumba yake ya awali iliyoathirika na maafa hayo, tarehe 30
Agosti, 2015.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,
Dkt. Florens Turuka akiagana na mwenyekiti Kijiji cha Mwakata wilayani
Kahama, Ezekieli Ramadhani mara baada ya kukagua ujenzi wa nyumba za
waathirika wa maafa ya mvua zilizojengwa na SUMA JKT, tarehe 30 Agosti,
2015, kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji SUMA JKT, Kanali Felix
Samillan na Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu,
Brig. Gen, Mbazi Msuya (mwenye kofia ).
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,
Dkt. Florens Turuka (mwenye miwani) na Mkuu wa Wilaya ya Kahama ( kulia
kwake), Benson Mpesya wakiwa katika picha ya pamoja na waratibu wa
shughuli za maafa Mwakata kutoka; Ofisi ya Waziri Mkuu, SUMA JKT, Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa Shinyanga, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kahama na
Halmashauri ya Msalala mara baada ya kikao cha ujenzi wa nyumba za
waathirika wa maafa ya mvua Mwakata, tarehe 30 Agosti, 2015
0 comments :
Post a Comment