Wasanii
wa Kundi la The W.D kutoka Temeke jijini Dar es Salaam, wakionyesha
umahiri wao wa kusakata dansi wakati wa robo fainali ya shindano la
Dance 100% 2015 lililofanyika kwenye viwanja vya Don bosco Oystebay
Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.Shindano hilo limeandaliwa na
EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania,Makundi 10 kati ya 15
yalifanikiwa kuingia katika kinyang’anyiro cha nusu fainali
zitakazofanyika hivi karibuni.
Vijana
wanaunda kundi la Timu Makorokoro wa wilaya ya Temeke jijijini Dar es
Salaam, wakikongo nyoyo za mashabiki waliojitokeza kwenye onyesho la
robof wa shininali ya shindano la Dance100%2015,lililofanyika kwenye
viwanja vya Don bosco Oysterbay mwishoni mwa wiki jijini Dar es
Salaam.Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom
Tanzania,Makundi 10 kati ya 15 yalifanikiwa kuingia nusu fainali
zitakazofanyika hivi karibuni.
Vijana
wanaaunda kundi la timu ya Shamba kutoka Temeke wakionyesha umahiri wa
kusakata dansi wakati wa robo fainali ya shindano la Dance 100%
lililofanyika kwenye viwanja vya Donbosco Oysterbay jijini Dar es Salaam
,mwishoni mwa wiki.Shindano hilo iliandaliwa na EATV na kudhaminiwa na
Vodacom Tanzania. Makundi 10 kati ya 15 yalifanikiwa kuingia nusu
fainali zitakazofanyika hivi karibuni.
Vijana
wanaounda kundi la The Winner Crews kutoka Kiwalani jijini Dar es
Salaam, wakikongo nyoyo za mashabiki waliojitokeza kwenye onyesho la
robofainali ya shindano la Dance100%2015,lililofanyika kwenye viwanja
vya Donbosco Oysterbay jijini Da res Salaam ambapo makundi 10 yalitinga
nusu fainali zitakazofanyika hivi karibuni. Shindano hilo limeandaliwa
na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Kundi
la wasichana pekee la Cute Babies kutoka Keko wilaya ya Ilala jijini
Dar es Salaam wakionyesha umahiri wao wa kudansi wakati wa robo fainali
ya shindano la Dance 100% lililofanyika katika viwanja Don bosco
Oysterbay jijini ambapo makundi 10 yalitinga nusu fainali
zitakazofanyika hivi karibuni, Shindano hilo liliandaliwa na EATV na
kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.Baadhi
mashabiki waliojitokeza kwenye viwanja vya Donbosco Oysterbay wilaya ya
Kinondoni jijini Dar es Salaam, wakifuatilia mchuano wa robo fainalai
ya shindano la Dance 100% 2015 lililoandaliwa na EATV nakudhaminiwa na
Vodacom Tanzania mwishoni mwa wiki makundi 10 kati ya 15 yalifanikiwa
kuingia nusu fainali zitakazofanyika hivi karibuni.
Makundi kumi kati ya makundi 15 yaliyoshiriki katika kinyang’anyiro cha
kuingia katika nusu fainali ya mashindano yanayokuwa kwa kasi hapa
nchini ya Dance 100% yanayoandaliwa na kituo cha televisheni cha East
Africa(EATV) chini ya udhamini wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom
Tanzania,yanaendelea ambapo mwishoni mwa wiki tulishuhudia hatua ya robo
fainali kufanyika katika uwanja wa Don Bosco Oysterbay jijini Dar es
Salaam na kushirikisha makundi 15 kutoka wilaya 3 za mkoa wa Dar es
Salaam.
Makundi yaliyofanikiwa kuingia nusu fainali ni Wazawa
Crew,Majokeri,Quality boys,The best,The best boys kaka zao,Team
Makorokocho,The winners, The W.D, Cute babies na Team ya shamba.Mratibu
wa mashindano hayo,Happy Shame,alisema kuwa katika kinyang’anyiro cha
robo fainali hiyo walipata makundi 10 hayo ambayo yameingia moja kwa
moja katika ngazi ya nusu fainali.
“Huu ni mwaka wa nne East Africa Televisheni tunaandaa mashindano haya
chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania na mwaka hadi mwaka mashindano
haya yamekuwa yakiongezeka kupata umaarufu na kuwavutia vijana wengi
kila kona ya nchi yetu ambao wamekuwa wakijitokeza kushiriki”Alisema
Shame.
Shame, aliongeza kwamba kundi litakaloibuka na ushindi katika mashindano
haya ambayo pia yamekuwa yakionyeshwa na kituo cha televisheni cha East
Afrika kila jumatano saa moja kamili usiku,litajishindia kitita cha
shilingi milioni 5.
Naye Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania ambao ni wadhamini wakuu wa
mashindano haya,Matina Nkurlu alisema kuwa Vodacom inatoa udhamini kwa
kutambua kuwa muziki na michezo ni maeneo ambao yanaweza kutoa ajira kwa
vijana na kuweza kuwakwamua kimaisha.
Alisema kuwa Vodacom inatambua kuwa jukumu la kukabiliana na tatizo la
ajira hapa nchini sio la serikali peke yake bali pia ni la watu wote
ikiwemo makampuni,taasisi za umma na za binafsi na ndio maana siku zote
imekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono jitihada za kupambana na
tatizo la ajira kupitia nyanja mbalimbali ikiwemo michezo , burudani na
huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo.
“Vodacom tunaamini kuwa vijana wanaweza kuleta mapinduzi makubwa katika
sekta mbalimbali iwapo watawezeshwa,hivyo tunadhamini mashindano haya
tukiamini kuwa vijana wenye vipaji wanaoshiriki wataweza kujitangaza na
kujulikana ambapo katika siku za usoni ni rahisi kujiajiri kupitia
katika sanaa”Anasema Nkurlu.
Aliwataka vijana waamke hususani wasichana wasibaki nyuma na watumie
fursa kama hizi ili waweze kujikomboa kiuchumi “Suala la ajira sio
kufanya kazi ofisini tu bali kuna njia nyingi za kujiajiri na kujipatia
mapato mojawapo ikiwa ni kupitia michezo,muziki na sanaa nyingine na
Vodacom siku zote tutakuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za
vijana kujikwamua kiuchumi”Alisisitiza Nkurlu.
0 comments :
Post a Comment