Mgombea Urais kupitia UKAWA ndugu Edward Lowassa akiwa na Mgombea
mwenza ndugu Juma Duni Hajii katika wa mkutano wa kumtambulisha jijini
Mwanza
Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe akihutubia mamia ya wakazi wa
Mwanza wakati wa kumtambulisha Mgombea wa UKAWA jijini Mwanza
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akihutubia Umati wa Wakazi wa Jiji la Mwanza uliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Furahisha, wakati wa Mkutano wa hadhara wa kutafuta wadhamini wa Tume ya Uchaguzi (NEC) kwa wagombea hao na kutambulishwa kwa wananchi, Agosti 16, 2015.
Umati wa Wakazi wa Jiji la Mwanza ukiwa umefurika kwa wingi katika Barabara kuu ya kutoka Uwanja wa Ndege kuelekea katikati ya mji, wakati wa mapokezi wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa,ambaye yupo kwenye ziara ya kutafuta wadhamini wa Tume ya Uchaguzi (NEC) na kutambulishwa kwa wananchi, leo Agosti 16, 2015.
Umati wa Wakazi wa Jiji la Mwanza ukiwa umefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Furahisha, kulikofanyika Mkutano wa hadhara wa kutafuta wadhamini wa Tume ya Uchaguzi (NEC) na kutambulishwa kwa wananchi, Agosti 16, 2015.
Sunday, August 16, 2015
MAELFU YA WAKAZI WA MWANZA WAMLAKI MH EDWARD LOWASSA
Mbali na kuwa na umati mkubwa wa wafuasi katika mikutano hiyo viongozi wa vyama vinavyounda umoja huo wameendelea kusistiza kuwa Watanzania wajitokeza kwa wingi wao siku ya kupiga kura na walinde kura zao na huku wakitoa matamko mbalimbali juu ya vyombo vya Ulinzi na Usalama kusimamia haki na kulinda usalama wa Watanzania sio kutumika na baadhi ya viongozi kwa maslahi yao binafsi na kuwa hali hiyo ikipuuzwa italeta machafuko katika Taifa.






















0 comments :
Post a Comment