Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kati Afrika wanaotokea nchini Tanzania, ameuawa na waasi huku wengine 18 wakijeruhiwa vibaya.
Kwenye Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Ulinzi Tanzania imesema kwamba tukio hilo limetokea Juni 3, 2018 huko Afrika ya Kati, ambapo kikosi hiko chenye askari 90 kilishambuliwa na waasi wanaojulikana kwa jina la Sirir, na kusababisha kifo cha askari huyo mmoja, kujeruhi 18 huku watano kati yao wakiwa katika hali mbaya zaidi.
Majeruhi wa shambulio hilo wamepelekwa katika Hospitali ya Kanda ya Umoja wa Mataifa iliyopo Bangui kupatiwa matibabu, huku utaratibu wa kuurejesha mwili wa marehemu nyumbani Tanzania zikiwa zinaendelea.
0 comments :
Post a Comment