Na Mwandishi Wetu
…………………………………..
MWIMBAJI wa muziki wa injili Rose
Mhando amethibitisha rasmi kushiriki katika Tamasha kubwa la kihistoria
la kuiombea Amani nchi kuelekea uchaguzi mkuu linarotarajia kufanyika
Oktoba 4 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaa kabla ya kwenda
mikoani.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa
maandalizi ya tamasha hilo Alex Msama, alisema Mhando tayari
amethibitisha kuimba siku hiyo, ambako tayari ameshaanza maandalizi
ikiwa pamoja na nyimbo mpya ambazo ni maalumu kwa ajili ya kuhamasisha
amani.
Msama alisema kuwa maandalizi ya
tamasha hilo la kihistoria yanaendelea vizuri ikiwa pamoja na waimbaji
kujiandaa vizuri watakuwepo waimbaji kutoka nchi zaidi ya tano kuungana
na watanzania katika tukio hilo ambalo litashirikisha matukio
mbalimbali.
Aidha Msama alisema kuwa mbali ya
kuliombea taifa amani kuelekea katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa
kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Alisema kuwa waimbaji wengine
wanaendelea kuthibitisha ambapo pia mbali ya kuimba mmojammoja wataimba
wimbo wa pamoja ambao umeandaliwa, hivyo Msama aliwaomba watanzania
kujitokeza katika tukio hilo muhimu la kitaifa.
Naye Mjumbe wa Kamati ya
maandalizi ya tamasha hilo, Beno John Chelele alisema tamasha hilo ni la
muhimu hasa katika kipindi hiki cha uhaguzi ambao umekuwa wa tofauti
na chaguzi zilizowahi kufanyika miaka ya nyuma.
“Kila Mtanzania ashiriki
tuliombee taifa letu kokote litakakopita tamasha hili ni la muhimu hasa
katika wakati huu wa uchaguzi ambao ni wa aina yake,” alisema Beno.
Tamasha hilo litanzia mkoa wa Dar
es Salaam Oktoba 4, Morogoro Oktoba 7, Iringa 9,Mbeya Oktoba 11, Dodoma
Oktoba 14, Shinyanga Oktoba 16 na kumaliziwa na Mwanza Oktoba 18.
0 comments :
Post a Comment