Vijana
watatu wakitanzania ambao kwa ubunifu mkubwa wameweza kuja na wazo
ambalo linatekelezeka katika ulimwengu wa teknolojia ya habari na
mawasiliano.
Inawezekana
ukaanza kutafuta na kuwaza kwamba inawezekanaje tango kuwa televisheni?
Hilo ni jina waliloweza kukipa king’amuzi chao kinachoitwa TangoTv.
Vijana
hawa wanakuja na teknolojia ya kisasa kabisa ya kukuwezesha wewe kuweza
kuangalia filamu zote za hapa Bongo na Afrika kwa ujumla, kupitia
kingamuzi chao hicho ambacho kinakupa huduma hiyo kwa kutumia mtandao wa
intaneti uliounganishwa moja kwa moja na king’amuzi chao, wala
hauhitaji antena.
Vile vile
inamaanisha kila sehemu hapa Tanzania ambayo unaweza kupata intaneti ya
simu kwa kuanzia 3G, huna shaka kabisa na king’amuzi hiki maeneo kama
hayo utapata huduma vizuri.
Vijana
hawa ambao wako watatu ambao wameingia kwenye vijana fursa ya kuwa
wabunifu bora 30 Afrika katika teknolojia,(Demo Africa Top 30)
na wanaipeperusha bendera ya Tanzania. Utofauti wa teknolojia yao ni
kwamba wao wameweza kukusanya filamu za kiafrika na kuhakikisha
unazipata kupitia king’amuzi chao ambacho kinatumia mtandao wa 4G. 3G,
Wifi na pale unapounganisha intaneti ya kawaida mahali popote na wakati
wowote.
Ukweli ni
kwamba si watu wengi wana uwezo wa kuangalia filamu za bongo au
kuzipata kwa urahisi ila kwa teknolojia hii inamaanisha unaweza
kuangalia kupitia king’amuzi chao ambacho kimeunganishwa na mtandao wa
intaneti huku kikikupa nafasi ya kufuatilia filamu kwenye Youtube.
Unaweza kulipia kwa kila filamu unayotaka au kwa mwezi n.k
Teknolojia
hii inafanya kazi kwenye televisheni za kawaida ambazo watanzania wengi
wanamiliki, cha zaidi ni kwamba unaweza kutumia Tango kwenye kompyuta
yako, simu yako n.k
Kuanza mradi huu wamewezeshwa na tume ya sayansi na teknolojia chini ya serikali ya Tanzania ili waweze kuonyesha bidhaa yao ya kwanza na kuweza kuiwezesha kufika sokoni. Kwa sasa unaweza kuweka oda yako kwenye mtandao wao wa www.tangotv.co.tz na hii inaashiria kitu kizuri katika mafanikio yao na teknolojia kwa ujumla wake hapa Tanzania.Kwa upande mwingine ni kwamba wanafanya kitu kipya ambacho ving’amuzi vingine haviwezi kufanya isipokuwa kimoja tu ambacho si cha hapa Tanzania, hiyo kuwapa fursa ya wao kuwa na kivutio kikubwa cha filamu cha Tanzania na zile za kuelimisha ambazo pia ni za kitanzania kwa ajili ya watoto.Je swali ni kwamba wasanii wa filamu za hapa bongo wanalijua hilo? Je wako tayari kunufaika na teknolojia hii ambayo vijana wameweza kuiwaza? Hii inamaanisha kwamba msanii anaweza kutengeneza kazi yake na kuiweka kwenye mtandao wao na kunufaika katika mauzo ya filamu zetu za hapa Bongo.

0 comments :
Post a Comment