@nkupamah blog
Mwenyekiti
wa umoja wa wanafunzi wahitimu wa darasa la saba Shule ya Msingi
Muhimbili Mwaka 1988, Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungumza.
Mwenyekiti
wa umoja wa wanafunzi wahitimu wa darasa la saba Shule ya Msingi
Muhimbili Mwaka 1988, Bi. Usia Nkhoma Ledama akionesha sehemu ya msaada
wa viti na meza na ofisi iliyokarabatiwa na umoja wao.
Mkuu
wa Shule ya Msingi Muhimbili wa sasa, Dafrossa Asenga (katikati)
akizungumza kuwakaribisha wageni katika hafla ya kukabidhiwa msaada wa
viti na meza vilivyotolewa na wanafunzi wahitimu wa darasa la saba Shule
ya Msingi Muhimbili Mwaka 1988.
Mwenyekiti
Msaidizi wa umoja wa wanafunzi wahitimu wa darasa la saba Shule ya
Msingi Muhimbili Mwaka 1988, akitoa machache katika hafla hiyo ya
kukabidhi msaada wa viti na meza na ofisi iliyokarabatiwa na umoja wao.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Muhimbili kwa sasa wakiwa katika hafla hiyo iliyofanyika shuleni hapo.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Muhimbili kwa sasa wakiwa katika hafla hiyo iliyofanyika shuleni hapo.
Baadhi
ya walimu wastaafu waliowafundisha wanafunzi hao wakijitambulisha
katika hafla hiyo ya kukabidhi msaada wa viti na meza walizotoa kwa
shule yao kama shukrani yao.
Baadhi
ya wanafunzi waliohitimu darasa la saba mwaka 1988 Shule ya Msingi
Muhimbili pamoja na wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya kukabidhi
msaada wa viti na meza walizotoa kwa shule yao kama shukrani yao.
Baadhi
ya walimu wastaafu waliowafundisha wanafunzi hao wakijitambulisha
katika hafla hiyo ya kukabidhi msaada wa viti na meza walizotoa kwa
shule yao kama shukrani yao.
Ernest
Nyambo ambaye ni Mweka Hazina wa Umoja wa waliohitimu wa darasa la saba
mwaka 1988 Shule ya Msingi Muhimbili akizungumza katika hafla hiyo.
Sehemu ya msaada huo wa viti vya kisasa 30, meza nane (9) vilivyokabidhiwa kama msaada shuleni hapo.
Sehemu ya msaada huo wa viti vya kisasa 30, meza nane (9) vilivyokabidhiwa kama msaada shuleni hapo.
Mgeni
rasmi wa hafla hiyo, Balozi Kassim Mwawado akizungumza katika hafla ya
kukabidhi msaada wa viti na meza vilivyotolewa na wanafunzi wahitimu wa
darasa la saba Shule ya Msingi Muhimbili Mwaka 1988.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Muhimbili ya sasa wakitoa burudani katika hafla hiyo.
Baadhi
ya wanafunzi waliohitimu darasa la saba mwaka 1988 Shule ya Msingi
Muhimbili pamoja na wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya kukabidhi
msaada wa viti na meza walizotoa kwa shule yao kama shukrani yao.
Na Mwandishi Wetu
WANAFUNZI waliohitimu darasa la
saba mwaka 1988 Shule ya Msingi Muhimbili wametoa msaada wa viti vya
kisasa 30, meza nane (9) na kufanya ukarabati ofisi ya walimu na ofisi
ya mwalimu mkuu wa shule hiyo ambapo gharama za msaada huo kwa pamoja
umefikia kiasi cha shilingi milioni 17.
Wakikabidhi msaada huo shuleni
hapo leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa umoja huo wa wanafunzi
wahitimu wa darasa la saba mwaka 1988, Bi. Usia Nkhoma Ledama alisema
wanafunzi hao wapatao 80 waliamua kuchangishana fedha na kuamua
kuisaidia shule yao ya zamani ikiwa ni kama shukrani kwa walimu na shule
iliyowapa elimu ya msingi.
Alisema katika msaada huo kuna
viti 29 na meza nane ambazo zimetengnezwa kisasa kwa ajili ya ofisi ya
walimu ‘staff room’, kiti na meza ya kisasa ya ofisi ya mwalimu mkuu wa
shule hiyo, pamoja na kufanya ukarabati wa ofisi ya walimu ikiwemo
kupaka rangi, kukarabati dirisha na kufunga feni ili ifanane na thamani
zilizowekwa.
Bi. Ledama alisema wanafunzi hao
ambao wameanzisha umoja huo kupitia mtandao wa jamii (whatsapp)baada ya
kukutana ndani ya miezi mitatu walikubaliana kufanya jambo moja la
kuisaidia chochote shule yao ikiwa ni ishara ya shukrani ndipo
walipofanya mawasiliano na kujua shule hiyo ilikuwa na uhaba wa viti
pamoja na meza za walimu hivyo kuchangishana hadi kupata msaada huo.
“…Baada ya mjadala katika kundi
letu la whatsapp kukubuka na kukumbushana maisha yetu ya shule ya msingi
kukolea ndipo tukapata wazo kutoa msaada kwa shule yetu ya msingi kama
alama ya shukrani yetu kwa malezi na elimu tuliopata hapa iliyoweza
kutufikisha hapa leo, tarehe 7 mwezi Aprili mwaka huu (2015) sie tuliopo
Dar es Salaam tukakutana kwa mara ya kwanza na kujadiliana namna ya
kusaidia shule yetu,” alisema Bi. Ledama.
Kwa upande wake Mgeni Rasmi wa
hafla hiyo, Balozi Kassim Mwawado aliwapongeza wanafunzi hao kwa kitendo
cha kuguswa na kuamua kuikumbuka shule waliosoma na kuwaomba waendelee
na moyo huo wa ushirikiano kwa masuala mbalimbali ili kujenga mshikamano
zaidi baina yao.
Aidha aliushauri uongozi wa shule
kuwa na eneo maalum la kuweka kumbukumbu kwa wanafunzi waliosoma shuleni
hapo na kufanikiwa pamoja na matukio muhimu ambayo yatawajengea
mwongozo mzuri wanafunzi na morali ya kufanya vizuri zaaidi katika
masomo yao.
Naye Mkuu wa Shule ya Msingi
Muhimbili wa sasa, Dafrossa Asenga akipokea msaada huo aliwashukuru
wanafunzi waliojitolea na kuwataka wauendeleze umoja wao huo ili uweze
kudumu na kushirikiana na kusaidiana kwa masuala mbalimbali ya msingi.
Hafla hiyo ya tukio la kukabidhi
msaada huo pia iliwakutanisha baadhi ya walimu waliowafundisha wanafunzi
hao mwaka 1988, baadhi ya wanafunzi waliohitimu darasa la saba mwaka
1988, viongozi wa bodi ya shule, pamoja na wanafunzi na walimu wa sasa
wa shule ya Msingi Muhimbili.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
0 comments :
Post a Comment