Baadhi
ya Wajasiriamali wakiwa katika maonyesho ya bidhaa mbalimbali kwenye
kongamano la wajasiriamali lililofanyika Hoteli ya Mbezi Garden mapema
mwaka huu. Kongamano la namna hiyo linatarajiwa kufanyika Septemba 26,
2015 jijini Mwanza Ukumbi wa Benki Kuu (BoT), Capripoint.
Na Dotto Mwaibale
WAJASIRIAMALI
zaidi ya 250 wanatarajia kuonyesha bidhaa zao mbalimbali katika
kongamano la mafunzo ya ujasiriamali litakalofanyika jijini Mwanza.
Akizungumza
na Dar es Salaam leo, Mratibu wa kongamano hilo, Getrude Kilyabusebu
alisema lengo la kongamano hilo ni kutoa mafunzo ya ujasiriamali ili
kuwajengea uwezo wajasiriamali hao.
"Wajasiriamali
hao katika kongamano hilo watapata fursa ya kuonesha bidhaa zao
mbalimbali na pia watapata mafunzo ya jinsi ya kukuza mitaji yao na
mbinu zingine za biashara" alisema Kilyabusebu.
Alisema
makongamano ya namna hiyo yamekuwa yakiwasaidia wajasiriamali hao
kujuana na kubadilishana uzoefu wa kibiashara na utengeneza wa bidhaa
zao zikiwemo mbinu za ufugaji na kilimo.
Alisema
mafunzo hayo utolewa na wataalamu waliobobea katika shughuli za
ujasiriamali na matunda ya mafunzo ya makongamano hayo yamewanufaisha
wajasiriamali wengi wajasiriamali.
Kilyabusebu
alisema kongamano hilo lililoandaliwa na Jumuiya ya Wanawake
Wajasiriamali Tanzania (Tanzania Business Entrepreneurs Women) lita
Septemba 6, 2015 jijini Mwanza katika ukumbi wa Benki Kuu (BoT)
Capripoint.
Mratibu
huyo alisema kuwa pamoja na mambo mengine kila mshiriki atalazimika
kuchangia gharama kidogo ili kufanikisha kongamano hilo ambapo katika
mafunzo na chakula atatakiwa kulipia sh.30,000, meza ya kuuzia bidhaa na
kuzitangaza sh. 20,000 na mafunzo na meza sh.50,000.
Kilyabusebu
alitumia fursa hiyo kuwaomba wajasiriamali wa kanda ya ziwa kuweza
kushiriki katika kongamano hilo ambalo ni muhimu kujifunza stadi za kazi
zao.
Kwa maelezo zaidi kuhusu kongamano hilo unaweza kupiga simu namba 0754032589 /0756334078/0673032589.

0 comments :
Post a Comment